Mahitaji Ya Dunia Na Ya Aakhera Kutimizwa Kwa Kumsalia Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Siku Ya Ijumaa

عن أنس بن مالك خادم النبي صلى الله عليه وسلم قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: إن أقربكم مني يوم القيامة في كل موطن أكثركم علي صلاة في الدنيا من صلى علي في يوم الجمعة وليلة الجمعة قضى الله له مائة حاجة سبعين من حوائج الآخرة وثلاثين من حوائج الدنيا ثم يوكل الله بذلك ملكا يدخله في قبره كما يدخل عليكم الهدايا يخبرني من صلى علي باسمه ونسبه إلى عشيرته فأثبته عندي في صحيفة بيضاء (شعب الإيمان، الرقم: ٢٧٧٣، وسنده ضعيف كما في القول البديع صـ ٣٢٩)

Sayyidina Anas Bin Maalik (radhiyallahu ‘anhu) ameripoti kwamba Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, wale miongoni mwenu wanao niswalia zaidi duniani watakuwa karibu na mimi siku ya qiyamah, kila wakati. Yoyote ambaye ananiswalia usiku wa ijumaa na mchana wa ijumaa, Allah subhaana wata’alah atatimiza haja zake mia moja, mahitaji sabini ni aakhera na mahitaji thelathini ni ya duniani. baada ya kuniswalia, Allah subhaana wata’alah atamkabidhi malaika ambaye ataniletea kaburini, kama vile zawadi imeletwa kwako. Malaika wananijulisha mtu aliye niswalia kwa kuniambia jina lake na family yake. Kisha natunza salaam kwangu kwenye kitabu cheupe.

NB: Imaam Bayhaq (rahimahullah) ameripoti hii hadith chini ya sura ya ambiyaa (alayhimus salaam) kuwa wako hai kaburini

Kuokolewa Kutoka Kwa Wanyama Pori Kupitia Kwa Kumsalia Nabii Wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

Imeripotiwa kuhusu shekhe Abul Hasan Shaazili (rahimahullah) kwamba wakati mmoja, alikuwa kwenye wanyama pindi wanyama pori walipo anza kumsogerea. Akiwa anaogopa kuwa hawa wanyama pori watamdhuru, mara moja aliamua kumsalia Nabii (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Sababu yake kufanya hivi ni kwamba Imeripotiwa kwenye hadith sahihi kwamba pindi mtu akituma salaam moja kwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam), Allah subhaana wata’alah anatuma salaam kumi (yaani rahma) kwake, na mtu ambaye Allah subhaana allah amempe rehma zake, Allah subhaana wata’alah anatoshereza kwa uoga wake wote na wakati mgumu atakao kutana nao. Kwa hivyo kumswalia Nabii wa allah (sallallahu ‘alaihi wasallam), shekhe Shaazili (rahimahullah) aliokolewa kutoka kwa wanyama pori. (Al-Qawlul Badee, Pg, 265)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …