قال النبي صلى الله عليه وسلم من صلى علي في يوم خمسين مرة صافحته يوم القيامة (القربة لابن بشكوال، الرقم: ٨٧، وقد سكت عنه السخاوي في القول البديع صـ ٢٨٩، ويفهم من سكوته أن الحديث معمول به عنده، ولذلك ذكره في كتابه)
Imeripotiwa kwamba Nabii (sallallahu alaih wasallam) amesema “yoyote atakaye niswalia mara khamsini kila siku, nitafanya musaafaha (kushikana mikono) na yeye siku ya mwisho.”
Njia ya kupata ukaribu wa Allah subhaana wata’alah
Ka’b Ahbaar (rahimahullah) (ni taab’ iee ambaye alikuwa miongoni mwa wasomi wa mayahudi aliyekubali uislaam) ameripoti:
Allah subhaana wata’alah alimuambia Moosa (alayhis salaam) kwa kusema, ewe Moosa, ukaribu zaidi na usemi wako ni kwa ulimi wako, ukaribu kupita maneno yako ni kwa ulimi, au hisia zako za ndani ziko kwa moyo wako au ukaribu kuliko roho yako ni mwili wako, au mboni za macho kwa macho yako? “Moosa (alayhis salaam) alijibu kwa kukubali. Allah subhaana wata’alah kisha alisema, kwahiyo soma salaamu kwa wingi kwa Muhammad (sallallahu alaih wasallam).” (Al-Qawlul Badee, Pg,270)