Sahaabah

Tamaa Ya Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) Kubarikiwa Na Chumba Kilichojaa Na Watu Kama Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) wakati fulani alikua amekaa pamoja na kundi la watu alipokuwa akiwahutubia na kuwauliza swali lifuatalo, “Niambieni nyinyi watu mnatamani kitu gani!” Mtu mmoja alisema: “mimi natamani chumba hiki kizima kijazwe na dirham (sarafu za fedha) na nizitoe zote katika Njia ya Allah Ta’ala.” Umar (Radhiya Allaahu …

Soma Zaidi »

Uaminifu Mkubwa Wa Abu Ubaidah bin Jarrah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kusilimu, watu wa Najraan walikuja kwa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na wakamwomba awapelekee mtu mwaminifu (anayeweza kuwafundisha Dini). Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akawaambia: لأبعثن إليكم رجلا أمينا حق أمين “Nitawatumia mtu mwaminifu, hakika ni mwaminifu sana.” Katika hatua hiyo, Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliokuwepo wote walitamani kuwa wapokezi …

Soma Zaidi »

Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akiwapa Watoto Zake Majina Baada Ya Mashahidi Wa Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum)

Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliwahi kutaja: “Hakika Talha bin ‘Ubaidillah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anatoa majina ya Ambiyaa (‘Alaihimus salaam) kwa watoto zake, ambapo anajua kwamba hakutokuwa Nabii atakayekuja baada ya Nabii Muhammad (Sallallahu ‘alaihi wasallam). Kisha Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Natoa majina ya mashahidi (wa Maswahaabah) kwa wanangu ili …

Soma Zaidi »

Ushujaa wa Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Siku ya (vita) vya Yarmuk, Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walimwambia Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu): “Kwa nini huwashambulia maadui kwa ijtihada zote, nasi tutakufuata katika kuwashambulia ?” Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Najua kwamba nikiwashambulia na ijtihada zote, nyinyi hamtaungana nami. Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wakasema, “Hapana, tutaungana nawe.” Zubair (Radhiya …

Soma Zaidi »

Ukarimu Wa Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Hishaam bin ‘Urwah anataja kwamba maswahaabah saba (Radhiya Allaahu ‘anhum) walimchagua Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa mtekelezaji wa mali zao baada ya kufariki kwao. Miongoni mwa hawa maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘anhu), ‘Abdur Rahmaan bin ‘Auf (Radhiya Allaahu ‘anhu), Miqdaad (Radhiyallahu ‘anhu) na ‘Abdullah bin Mas’uud …

Soma Zaidi »

Istiqaama Katika Uislamu

Abul Aswad anasimulia yafuatayo: Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisilimu na umri wa miaka minane, na akafanya hijrah akiwa na umri wa miaka kumi na nane. Mjomba wake alikuwa akimweka ndani la kibanda kidogo na kuwasha moto ili ateseke na moshi huo. Kisha mjomba wake angemuamuru kuu achana Uislamu, ambao alikuwa …

Soma Zaidi »

Kushiriki katika Vita vya Badr

Ismaa’il bin Abi Khaalid anasimulia kwamba Bahiyy (rahimahullah) alisema: “Wapanda farasi walikuwa wawili tu wakipigana katika Jihaad kwenye tukio la Badr. Mmoja wao alikuwa Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu), ambaye alikuwa akipigana upande wa kulia, na mwingine alikuwa Miqdad bin Aswad (Radhiya Allaahu ‘anhu), ambaye alikuwa akipigana upande wa kushoto. Hishaam …

Soma Zaidi »

Tahadhari katika kusimulia Hadith kutoka kwa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)

Abdullah bin Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba wakati fulani alimuuliza baba yake, Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu), “Kwa nini usimuli mahadith za Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam), kama vile maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wengine?” Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Sikuacha upande wa Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) baada ya kusilimu (yaani nina …

Soma Zaidi »