عن أوس بن أوس قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: إن من أفضل أيامكم يوم الجمعة فيه خلق آدم وفيه قبض وفيه النفخة وفيه الصعقة فأكثروا علي من الصلاة فيه فإن صلاتكم معروضة علي قال: قالوا: يا رسول الله وكيف تعرض صلاتنا عليك وقد أرمت يقولون بليت فقال: إن الله عز وجل حرم على الأرض أجساد الأنبياء (سنن أبي داود، الرقم: 1047، وقال الحاكم في مستدركه، الرقم: 1029: هذا حديث صحيح على شرط البخاري ولم يخرجاه وأقره الذهبي)
Aws bin Aws (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Miongoni mwa siku zenu bora ni siku ya Ijumaa. Siku ya Ijumaa Aadam (alahis salaam) aliumbwa, siku ya Ijumaa alifariki duniani, siku ya Ijumaa baragumu litapulizwa, na siku ya Ijumaa viumbe vyote vitapoteza fahamu. Basi zidisheni kuniswalia siku ya Ijumaa kwa sababu salaa na salaam zenu zinaletwa kwangu.” Maswahaba wakauliza, ‘Ewe Mtume wa Allah (sallallahu alaihi wasallam)! Vipi salaa na salaam zetu zitakufikiya ikiwa mwili wako utakuwa umeoza kaburini?’ Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akajibu, ‘Hakika Allah subhaana wata’ala ameharamisha ardhi kula miili za manabii (sallallahu ‘alaihi wasallam).’”
Kutoka kwa ‘Qoot-ul-Quluub’, Allaamah Sakhaawi (rahimahullah) ananukuu kwamba ‘salaa na salaam kwa wingi’ iliyotajwa katika Hadithi hapo juu, inamaanisha kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) angalau mara mia tatu kila siku. Moulana Rashid Ahmad Gangohi (rahimahullah) pia aliwaagiza wafuasi wake kutuma salaa na salaam juu ya Nabii (sallallahu alaihi wasallam) mara mia tatu.
Zainul Aabideen, Ali bin Husein (rahimahullah), aliwahi kusema: Sifa kuu ya wale wanaofungamana na Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah ni kumswalia Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) kwa wingi”
Ubora wa Usiku juu ya mchana
Katika Nuzhatul Majaalis, hadithi ya kushangaza imesimuliwa kuhusu mjadala uliofanyika kati ya usiku na mchana, kila mmoja wao akijaribu kuthibitisha wema wake juu ya mwingine.
Mchana alimwambia usiku, “Mimi ni mbora kuliko wewe. Swalaah tatu za faradh Zinanaswaliwa ndani mwangu na swala mbili tu zinaswaliwa ndani yako. Nina wakati wa kukubaliwa siku ya Ijumaa ambayo hakuna mtu anayemuomba Allah subhaana wata’ala kwa chochote isipokuwa anajaliwa.
Saumu za Ramadhaan zinazingatiwa kwangu pia. Wewe ni wakati tu wa kulala na wakati ambapo watu wameghafilika. Mimi nimewekewa na kukesha na shughuli, na kuna baraka kubwa katika kuwa kushughulika. Jua pia huchomoza ndani mwangu na kuleta mwanga katika dunia nzima.”
Usiku alijibu kwa kusema, “Ikiwa unajivuna juu ya jua, basi mimi na zingatia kwamba nyoyo za wanao simama kuswali usiku na nyoyo za wanao fikiri juu ya hekima iliyo nyuma ya uumbaji wa Allah subhaana wata’ala kuwa kubwa zaidi kuliko jua. Unawezaje kufikia furaha ambayo wapenzi hupata wakati wako peke yangu na mimi? Jinsi gani unaweza kujilinganisha na Usiku wa Mi’raaj? Una jibu gani kwa amri ya Allah subhaana wata’ala kwa Mtume Wake (sallallahu alaihi wasallam) aliposema, ‘Na kutoka (sehemu ya) usiku, swali humo kama kitendo cha ziada.’ Allah subhaana wata’ala ameniumba kabla yako. Nina Usiku wa qadr (yaani Lailatul Qadr) ambao Allah subhaana wata’ala Hujaalia Fadhila nyingi. Allah subhaana wata’ala anaita katika sehemu ya mwisho ya usiku, ‘Je! kuna yoyote atakaye niomba ili niimpe? Je! Kuna yoyote anayeomba msamaha nimsamehe?’ Kwani hufahamu kuwa Allah subhaana wata’ala Amesema ‘Ewe mwenye kujifunga (ndani ya shali)! Simama (kuswali) usiku kucha kasoro kidogo tu!’ Je, hukumsikia Allah subhaana wata’ala akisema, ‘Ametakasika ambaye alimchukua mja wake usiku kutoka Musjid Al-Haraam hadi Musjid Al-Aqsa?”. (Nuzhatul Majaalis 90/2)