عن أبي الدرداء رضي الله عنه قال قال رسول الله صلى الله عليه و سلم من صلى علي حين يصبح عشرا وحين يمسي عشرا أدركته شفاعتي يوم القيامة رواه الطبراني بإسنادين أحدهما جيد (الترغيب و الترهيب رقم 987)
Sayyidina Abu Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kasema, “Mwenye kuniswalia mara kumi asubuhi na jioni mara kumi, atapata ukombozi wangu siku ya qiyaamah.”
Mwandishi wa swala na salaam
Sheikhul Hadith Molana Muhammad Zakariyya (rahimahullah) ameeleza:
Rafiki yangu wa kutegemewa alinifahamisha kuhusu mwandishi wa Lucknow (sehemu). Alikua akianza kazi yake ya kila siku baada ya kuandika salaa na salamu kwenye karatasi ambayo alikuwa ameihifadhi kwa ajili hiyo.
Wakati wa kifo chake, aliingiwa na khofu ya Akhera akisema: “Ni nini kitanipata baada ya mimi kuondoka hapa duniani?” Aliposema hivi, majzob (Mchamungu ambaye anashughulika mara kwa mara katika kumkumbuka Mwenyezi Mungu) alitokea na kusema, “mbona una wasiwasi sana?
Karatasi (ambayo uliandika juu yake salaa na salaam) iko kwa Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na inapambwa.” (Fadail e Durood, Pg, 153)