Matokeo ya mkusanyiko usio na Dhikr na saalat na salaam

عن جابر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ما اجتمع قوم ثم تفرقوا عن غير ذكر الله وصلاة على النبي صلى الله عليه وسلم إلا قاموا عن أنتن جيفة (مسند أبي داود الطيالسي، الرقم: 1863، ورواته ثقات كما في إتحاف الخيرة المهرة، الرقم: 6062)

Imepokelewa kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Kila kundi la watu linapokusanyika na baada ya hapo likasitisha mkusanyiko wao na kuondoka bila ya kufanya Dhikr ya Allah subhaana wata’ala au Kumswalia Nabii wa Allah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwenye hicho kikao ni kama wamemkusanyikia maiti mwenye harufu mbaya kisha wakaondoka (yaani mkusanyiko usiokuwa wa Dhikr au salaa na salaam ni kitu kibaya sana ambalo linafananishwa na harufu mbaya ya maiti ambayo hakuna mtu anayetaka kuisogelea).”

Kuongeza ‘Salaam’ katika salaa na salaam

Abu Sulaimaan Haraani (rahimahullah) anasema:

Siku moja nilimuona Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika ndoto akaniambia, “Ewe Abu Sulaimaan, unaponakili Hadith na kutajwa jina langu, naona kwamba unatosha kuswali na hunitumii ‘salaam’ (yaani wasallam) ni neno lenye herufi nne, na kwa kila herufi moja litakupokea thawabu mara kumi (yaani thawabu arobaini za ziada). kwa nini basi unatupa thawabu arobaini? (Al Qawlul Badee, Pg,488)

About admin

Check Also

Chanzo cha nuru siku ya Qiyaama

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم زينوا …