Dalili Za Qiyaamah Part 4

Dalili Kumi Kubwa Za Qiyamah

Kama jinsi kuna dalili nyingi ndogo za Qiyaamah zilizorekodiwa katika Ahaadith, hivyo hivyo kuna dalili nyingi kubwa ambazo pia zimetajwa katika Ahaadith. Dalili hizi kubwa ni matukio muhimu ambayo yatatokea ulimwenguni kabla ya Qiyaamah na itatangaza ukaribu wa Qiyaamah. Muhadditheen wame eleza kuja kwa Mahdi (Radhiyallahu ‘Anhu) ni dalili ya kwanza ya Qiyaamah. (Ishaa’ah pg. 191)

Katika dalili hizi kubwa za Qiyamah, kuna dalili kumi ambazo zimeelezwa na Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) katika Hadith ifuatayo. Ikiwa mtu atatafakari juu ya dalili hizi kumi, atatambua kuwa ni ya ukubwa kiasi kwamba athari zake zitaingia ulimwengu wote au sehemu kubwa nyingi ya ulimwengu.

Huzaifah bin Usaid (Radhiyallahu ‘Anhu) anaripoti, “Katika tukio moja, Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) alitujia sisi maswahaabah (Radhiyallahu ‘Anhum), wakati tukishiriki katika majadiliano. Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) aliuliza kutoka kwetu, “Mnajadili nini?” Tulijibu, “Tunazungumzia kuhusu tukio la Qiyaamah.” Kusikia haya, Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) alisema, “Kwa kweli, Qiyaamah haitatokea kamwe hadi utaona kabla yake dalili kumi kubwa. ”

“Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) kisha akataja dalili hizi kumi kuwa: moshi (hii ni aina ya ukungu au moshi ambao utashuka duniani kutoka angani ambayo Waislamu watapata homa na makafiri watazimia), Dajjaal kutokea, mnyama kutokea, jua kutoka magharibi, Nabi Isa (‘Alaihis Salaam) kushuka, Yajooj na Ma’jooj kutokea, ardhi kuzama mara tatu duniani; Kuzama mashariki, kuzama magharibi na kuzama katika peninsula ya Arabia. Dalili ya mwisho itakuwa moto ambao utatokea Yemen na kuwaongoza watu kuelekea katika uwanja wa kufufuliwa (Syria). ” (Saheeh Muslim #2901)

Katika dalili hizi kumi kubwa zilizotajwa katika Hadith hii, ya kwanza kutokea itakuwa kutokea kwa Dajjaal.

About admin