Sunna na Aadaab za Jumu’ah 4

12. Jitahidi kumswalia Mtume (sallallahu alaihi wasallam) mara elfu moja siku ya Jumu’ah.

Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Yule ambaye ananitumia salaa na salaam mara elfu moja siku ya Jumu’ah, hatofariki hadi atakapoonyeshwa makazi yake peponi.”[1]

13. Ni Sunnah kusoma Surah A’ala (sabbihisma rabbikal a’laa) katika Rakaah ya kwanza ya swala ya Jumu’ah na Surah Ghaashiyah (hal ataaka hadithul ghaashiya) katika Rakaah ya Pili. Pia ni Sunnah kusoma Surah Jumuah katika Rakaah ya kwanza ya Jumu’ah na Surah Munaafiqoon katika Rakaah ya Pili.[2]

14. Soma Surah kahf kabla au baada ya swala ya Jumu’ah. Katika riwaaya moja, kisomo cha Surah Kahf husababisha madhambi madogo ya wiki iliyopita kusamehewa.

Ibnu Umar (Radhiyallahu anhuma) anasimulia kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, “Yule anayesoma Surah Kahf siku ya Jumuah, Noor (mwanga) hutoka chini ya miguu yake na hadi angani. Noor hio itamwangaza siku ya Qiyaamah, na madhambi zake zote (ndogo) zilizofanywa kati ya Jumu’ah mbili zitasamehewa. “[3]

15. Inaruhusiwa kuomba dua moyoni mwako kati ya khutbah mbili. Haupaswi kuinua mikono yako au kuomba dua kwa midomo wakati huu.


[1] أخرجه ابن شاهين بسند ضعيف كذا في القول البديع صـ 397

[2] عن سمرة بن جندب رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يقرأ فى صلاة الجمعة سبح اسم ربك الأعلى و هل أتاك حديث الغاشية (سنن أبي داود، الرقم: 1125)

عن ابن عباس أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يقرأ في صلاة الفجر يوم الجمعة: الم تنزيل السجدة، وهل أتى على الإنسان حين من الدهر وأن النبي صلى الله عليه وسلم كان يقرأ في صلاة الجمعة سورة الجمعة والمنافقين (صحيح مسلم، الرقم: 879)

[3] رواه أبو بكر بن مردويه في تفسيره بإسناد لا بأس به كذا في الترغيب والترهيب، الرقم: 1098، وقال الحافظ في نتائج الأفكار 5/42:  هكذا أخرجه الضياء في المختارة ومقتضاه أنه عنده حسن وفيه نظر وكذا ذكر المنذري في التغريب أنه لا بأس بإسناده فإما خفي عليهما حال خالد بن محمد فقد تكلم فيه ابن منده وإما مشياه لشواهده

About admin