Hofo Ya Abdur Rahman bin Auf (Radhiyallahu ‘Anhu) Kutoa Hesabu

Naufal bin Iyaas Al Huzali (Rahimahullah) anasimulia:

‘Tulikuwa tukikaa na Abdur Rahman bin Auf (Radhiyallahu’ Anhu), na alikuwa ni rafiki mzuri sana. Siku moja, alitupeleka nyumbani kwake kula. Wakati tulikaa chini na sahani ya chakula iliyo na nyama na mkate ililetwa mbele yetu, alianza kulia.

Tulimuuliza, “Ni nini kinachokusababisha kulia ehh Abu Muhammad?” Akajibu, “Sababu ya mini kulia ni kwamba Rasulullah (Sallallahu ‘Alaihi Wasallam) aliiacha dunia kwa hali kwamba yeye wala familia yake hawakula mkate hadi kujaza tumbo zao (wakati wa uhai wake). Ninaogopa isiwe kuwa kwamba tunaachwa nyuma (ulimwenguni ili kufurahiya fadhila hizi) na badala ya hili, tutanyimwa fadhila za Akhera.” (Isaabah 4/292)

About admin

Check Also

Kusherehekea mwaka mpya

Swali: je inajuzu kutakiana “heri ya mwaka mpya” mwaka mpya wa kiingereza unapoanza? Baadhi ya …