Abdur-Rahman bin Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akiongoza Swalaah.

Wakati wa safari ya Tabook, Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walikuwa wakisafiri pamoja na Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam). Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliwaacha Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) kwenda kujisaidia.

Kwa vile hakukuwa na muda mwingi uliobakia kwa Swalah ya Alfajiri, na Maswahabah (Radhiya allahi ‘anhum) waliogopa kwamba muda wa swalaah ungepita, hawakumngojea Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), lakini walimwomba Abdur-Rahman bin Auf (Radhiya Allaahu ‘anhu) awaongoze katika swala ya fajr.

Abdur-Rahman ibn Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikubali na akaanza kuswalisha. Wakati yeye alikuwa akiongoza swala, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akarudi na kujiunga na Swalaah. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisimama kwenye saf nyuma ya Abdur-Rahman ibn Awf (Radhiyallahu ‘anhu).

Baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) walianza kusoma tasbihi ili kumfahamisha Abdur-Rahman bin Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) amerudi na yeye arudi nyuma ili Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aende mbele na kuongoza Swalaah.

Abdur-Rahman bin Awf (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipotambua kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikuwa amesimama nyuma, alikusudia kurudi nyuma, lakini Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akamuashiria kwa mkono wake abaki pale alipo na aendelee kuswalisha.

Baada ya kumaliza Swalah, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliwaambia Maswahabah (Radjiyallahu ‘anhum) akisema, ‘Mmefanya vyema au akawaambia, “Mmefanya kwa usahihi (kwa kuanza Swalaah na humkuningojea.” Kwa maneno mengine, maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) walikuwa wanawasiwasi wakati huo kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) atakuchukizwa nao kutokana na wao kutokumgojea, lakini Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) aliwafariji kwamba katika hali kama hiyo, walikuwa wamefanya jambo sahihi.

About admin

Check Also

Kupokea jina la Al-Fayyadh kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam)

Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alimpa Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) cheo cha Talhah Al-Fayyaadh (mtu mkarimu …