6. Ni vizuri kuvaa nguo nyeupe.
Imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbaas (radhiyallahu anhuma) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Vaa nguo nyeupe, kwa sababu hiyo ni nguo bora kabisa, na wafunike humo marehemu zenu.”
7. Imepokewa kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) wakati fulani alikuwa akisoma Surah Sajdah katika rakaa ya kwanza na Surah Dahr katika rakaa ya pili ya Swalah ya Alfajiri siku ya Jumu’ah. Hivyo basi, mara moja moja mtu anapaswa kusoma Sura hizi katika Swalah ya Alfajiri siku ya Jumaa.
8. Nendeni mapema msikitini kwa ajili ya Swalah ya Jumu’ah. Kadiri mtu anavyoenda mapema, ndivyo thawabu anayopokea.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Mtu anayefanya ghusl kama ghusl ya janaabah (yaani. anajitakasa kabisa kwa namna ya mtu kujisafisha anapofanya ghusl kutoka janaabah, na baada ya hapo akaenda msikitini kwa ajili ya Swalaah ya Jumu’ah katika nafasi ya kwanza, basi atapata malipo sawa na yule anayetoa ngamia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), na atakaye kwenda kuswali Jumu’ah katika nafasi ya pili, basi atapokea malipo sawa na yule anaye chinja ng’ombe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mwenye kwenda kuswali katika nafasi ya tatu, basi anapata thawabu sawa na mwenye kuchinja kondoo mwenye pembe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah), na mwenye kwenda kuswali katika sehemu ya nne, basi anapata ujira sawa na yule anaye chinja kuku kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) , na mwenye kwenda kuswali Jumu’ah katika nafasi ya tano na ya mwisho, basi anapokea malipo sawa na yule anayetoa yai katika sadaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).