1. Soma Surah Dukhan siku ya Alhamisi usiku.
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu anhu) kuwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kusoma Surah Haa-mim Ad Dukhaan usiku wa kuamkia Alhamis atasamehewa madhambi yake.”[1]
2. Oga (fanya ghusl) siku ya Ijumaa. Yule ambaye ataoga siku ya Ijumaa, madhambi yake madogo yamesamehewa.
Imepokewa kutoka kwa Abu Bakr Siddiq (radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Mtu anayefanya ghusl siku ya Jumu’ah, dhambi zake ndogo husamehewa.”[2]
3. Ondoa nywele zisizohitajika na ukate kucha zako siku ya juma’ah.
4. Safisha kinywa chako na miswaak na upake manukato.
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’eed Khudri (Radhiyallahu anhu) kwamba Mtume (sallallahu alaihi wasallam) alisema: “Kila aliye baligh anatakiwa kufanya ghusl siku ya Jumu’ah, atumie miswaak na atumie manukato anayoweza kuitumia.”[3]
5. Vaa nguo zako nzuri zaidi siku ya Juma’ah.
Abdullah bin Salaam (radhiyallahu) anaripoti kwamba alimsikia Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akitoa khutbah siku ya Jumu’ah, “Kwa nini hununui nguo na kuiweka kwa ajili ya kuvaa siku ya Jumu’ah pekee yake, mbali na kuvaa nguo ya kawaida ya kila siku.?”[4]
[1] سنن الترمذي، الرقم: 2889، وقال: هذا حديث غريب
[2] شعب الإيمان للبيهقي، الرقم: 2760، قال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 3061: رواه الطبراني في الكبير والأوسط وفيه الضحاك بن حمرة ضعفه ابن معين والنسائي وذكره ابن حبان في الثقات
[3] صحيح مسلم، الرقم: 846
[4] سنن ابن ماجة، الرقم: 1095، صحيح ابن حبان، الرقم: 2777