Miongoni mwa fadhila za thamani za Allah Ta’ala juu ya mwanadamu ni fadhila ya watoto. Fadhila za watoto ni miongoni mwa neema maalum za Allah Ta’ala zilizotajwa katika Quraan Majeed. Allah Ta’ala anasema:
وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ
Allah Ta’ala amekuumbieni wake zenu katika nafsi zenu, na amekuumbieni wana na wajukuu katika wake zenu, na akakuruzukuni na riziki safi.
Neema nyingi za Allah Ta’ala ni kwamba manufaa na kheri zao ziko kwenye maisha ya mtu. Lakini, faida ya watoto ni uwekezaji kama huo hautoi wema tu kwa mtu katika maisha yake, lakini pia unaendelea kumnufaisha baada ya kifo chake.
Lakini, uwekezaji huu utaongeza tu wema kwa mtu ,ikiwa ataweka maadili ya deeni kwa watoto wake na kuwaunganisha na Allah Ta‘ala kama tu watoto wake wanashikilia Dini katika maisha yao na kutekeleza mafundisho ya Dini ambayo alikuwa amewapa, uwekezaji wake utaendelea kumletea wema na thawabu, hata baada ya kufariki kwake.
Kitu Bora Zaidi Mtu Anachoweza Kuacha Baada Ya Kufariki Kwake
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Vitu bora ambavyo mtu anaweza kuviacha baada ya kufariki kwake ni vitatu; mtoto mchamungu anayemuombea dua, sadaqat-ul-jaariyah (matendo mema – ambayo thawabu zake zinaendelea kumfikia mtu baada ya kufariki kwake), na elimu ya dini (aliyowanufaisha watu) ambayo watu wanaendelea kuyatenda yale mazuri baada ya kifo chake.
Katika Hadith nyingine, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Hakuna baba anayeweza kumpa mtoto wake zawadi bora kuliko zawadi ya tabia njema.”
Katika Hadith nyingine, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) ametaja: “Watendeeni watoto wenu kwa heshima na utu, na wafundisheni maadili mema.
Amri ya Quraan Majeed
Kuweka maadili ya deeni ndani ya watoto wetu ni muhimu sana na wajibu juu ya wazazi ambapo Allah Ta’ala amewaamrisha kutekeleza wajibu huu katika Quran Majeed. Allah Ta’ala anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا
Enyi mlio amini! Jiokoeni nafsi zenu na ahali zenu na moto wa Jahannum…
Kwa maneno mengine, unapaswa kuwaongoza wake zako na watoto wako kwenye Dini na kuwalinda kukanyaga njia ya upotofu. Kwa hivyo, Siku ya Qiyaamah, mtu pia ataulizwa kuhusiana na wajibu huu.
Kila Mzazi Anajukumu Na Ataulizwa Kuhusu Kizazi chake
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) amesema: “Kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu kundi lake. Kiongozi wa Kiislamu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake, na mume ni mchungaji ambaye ataulizwa kuhusu nyumba yake, na mke ni mchungaji nyumbani kwa mumewe na ataulizwa kuhusu kizazi chake…”
Kinyume chake, ikiwa mtu atapuuza kuwapa watoto zake malezi sahihi ya Kiislamu, na kushindwa kuingiza maadili ya deeni ndani wao, au hajali kuhusu marafiki na kundi la watoto zake, na kuwaruhusu kuwa na vitu vibaya, basi badala ya wao kuwa manufaa na kheri watakuwa msiba kwake katika dunia hii na ijayo.
Dua ya Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) na Nabii Dawud (alaihis salaam)
Imepokewa kwamba miongoni mwa dua ambazo Mtume (sallallahu alaihi wasallam) kazifanya kwa ajili ya ulinzi wa watoto waasi ni hizi zifuatazo:
اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنْ جَارِ السُّوْءِ وَمِنْ زَوْجٍ تُشَيِّبُنِيْ قَبْلَ الْمَشِيْبِ وَمِنْ وَلَدٍ يَكُوْنُ عَلَيَّ رَبًّا
Ewe Mwenyezi Mungu! Najikinga Kwako kutokana na jirani muovu, na mke ambaye atafanya nywele zangu kuwa nyeupe kabla ya uzee, na kutoka kwa mtoto ambaye atanitawala (kwa hivyo kunisababishia maumivu).
Vile vile, imepokewa kwamba miongoni mwa dua ambazo Nabii Dawood (alaihis salaam alikuwa akifanya ilikuwa:
اَللّٰهُمَّ إِنِّيْ أَعُوْذُ بِكَ مِنْ مَّالٍ يَكُوْنُ عَلَيَّ فِتْنَةً وَمِنْ وَلَدٍ يَكُوْنُ عَلَيَّ وَبَالًا
Ewe Mwenyezi Mungu! Naomba ulinzi Wako kutokana na mali ambayo itakuwa fitnah (mtihani) kwangu, na kutoka kwa mtoto ambae atakuwa ni balaa kwangu!
Kupitia hadith zake tukufu na mwenendo wake tukufu, Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) aliwafundisha Maswahaba na Ummah namna ya kuwapa watoto wao maadili mema ya dini na kuwapa adabu za kiislamu.
Kumfundisha Mtoto Maadili Mazuri Katika Hali Tofauti Za Maisha
Kuna vipimo vingi vya maisha ambavyo vinahitaji kuzingatiwa wakati wa kumfundisha mtoto maadili mazuri na adabu.
Baadhi ya vipimo hivi ni:
1. Kumfundisha mtoto imani sahihi za Kiisilamu na kuimarisha Imaan wake
2. Kumfundisha mtoto umuhimu wa kutimiza haki za Mwenyezi Mungu na kujiepusha na madhambi
3. Kumvutia mtoto umuhimu wa kutimiza haki za viumbe.
4. Kufundisha mtoto heshima, adabu na tabia nzuri Wakati wa kujiunga na watu.
5. Kumuelewesha mtoto umuhimu wa usafi wa nje na wa ndani.
6. Kuunda Hayaa na hofu ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).
7. Kusisitiza kwa mtoto umuhimu wa kuwa na marafiki wazuri kila wakati na kujiepusha na marafiki wabaya.
8. Kumfundisha mtoto njia maalum za kupata rahma za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah).