Mke wa Talhah (rahdiyallahu ‘anhu), Su’da bint ‘Awf al-Muriyyah alitaja tukio lifuatalo kuhusu mumewe Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu):
“Siku moja, Talhah aliingia nyumbani katika hali ya dhiki. Nilipoona hali hii, nilimwambia, ‘Kwa nini ninakuona ukiwa na huzuni? Kuna nini? Je! nilifanya jambo ambalo limekuuzi hadi nakuona ukiwa umefadhaika? Tafadhali niambie ili niweze kuondoa dhiki yako.’
Akajibu, ‘Hapana, hujafanya chochote ambacho kimeniumiza na kwa hakika wewe ni rafiki bora katika maisha ya Muislamu kama mimi.
Kisha nikamuuliza, ‘Nifafanulie ni jambo gani linalokuletea taabu.’
Akaniambia, ‘Mali niliyonayo katika milki yangu imeongezeka na hili limekuwa mzigo mkubwa kwangu.
Kisha nikamfariji nikisema, ‘Hakuna haja ya wewe kuwa na wasiwasi. Kwa nini usiigawe kati ya maskini?’
Talhah (rahdiyallahu ‘anhu) kisha akaanza kuigawa miongoni mwa masikini mpaka ikabaki dirham moja.”
Talhah ibn Yahya (rahimahullah) ametaja, “Nilimuuliza mweka hazina wa Talhah (radhiyallahu ‘anhu), ‘Talhah (radhiyallahu ‘anhu) aligawa mali ngapi wakati huo?’ Akajibu, ‘Aligawa dirham laki nne (miongoni mwa masikini wakati huo).” (Hilyatul Awliyaa 1/88)