Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akitimiza Ahadi Yake

Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaripoti:

Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) siku moja walimwambia bedui mmoja, “Nenda ukaulizie kutoka kwa Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kuhusu nani Allah Ta’ala Anayemkusudia (katika Aya ifuatayo ya Qur’an Majeed) “Miongoni mwao (Maswahaba) wapo waliotimiza ahadi zao (kwa Allah Ta’ala wa kubaki imara kwenye uwanja wa vita wakiwa tayari kujitolea maisha yao kwa ajili ya Dini).

Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) hawakuwa na ujasiri wa kumuuliza (Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) moja kwa moja kutokana na heshima kubwa kwake. (Kwa hivyo wakamwomba yule bedui amulize Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kwa niaba yao).

Bedui alipomuuliza Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) hakujibu. Bedui aliuliza swali kwa mara ya pili na ya tatu, lakini Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alikaa kimya.

Talha (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasema:

Kisha niliingia Msikitini huku nikiwa nimevaa kanzu ya kijani. Wakati Mtume (Sallallahu alaihi wasallam aliniona, akasema: “Yuko wapi mtu ambaye aliuliza kuhusu (Aayah ambayo Allah Ta’ala ametaja) “Wale ambao walitimiza ahadi yao (pamoja na Allah Ta’ala ya kubaki imara kwenye uwanja wa vita wakiwa tayari kutoa maisha yao kwa ajili ya Dini)?”

Bedui akajibu: “Mimi ndiye niliyeuliza, ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).

Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema: “Mtu huyu (akimaanisha Talhah) (Radhiya Allaahu ‘anhu)) ni miongoni mwa watu waliotekeleza ahadi yao (pamoja na Allah Ta’ala ya kubakia imara kwenye uwanja ya vita wakiwa tayari kutoa maisha yao kwa ajili ya dini).”

About admin

Check Also

Ukarimu Wa Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Ali bin Zayd (rahimahullah) anasimulia kwamba wakati fulani, Bedui mmoja alimwendea Talhah (Radhiyallahu ‘anhu) ili …