Jaabir bin Abdillah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia:
Siku ya Uhud, Maswahaba walipoanza kukimbia kutoka kwenye uwanja wa vita, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliachwa peke yake mahali fulani na maswahaabah kumi na mbili tu waliokuwepo pamoja naye. Miongoni mwa maswahaabah kumi na mbili alikuwepo Talhah ibn Ubaydillah (Radhiya Allaahu ‘anhu).
Wakati Mushrikeen waliposonga mbele kuelekea kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na wale maswahaabah kumi na mbili, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akageuka (kwa Maswahaba kumi na mbili) na akasema: “Nani kati yenu atatangulia kupigana na watu hawa?”
Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Nitapigana nao.”
Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Baki hapa (pamoja na mimi).”
Kisha Swahaabi mmoja wa Answaari akasema: “ mimi nitapigana nao, ewe Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam).
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Wewe nenda.” swahabi huyo alipigana mpaka akauawa kishahidi.
Wa Mushrikeen walisonga mbele kwa mara ya pili. Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) aliwqgeukia maswahaabah na akawauliza kwa mara ya pili: “Ni nani atakayepigana na watu hawa na kutulinda sisi?”
Talha (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema tena: “Nitapigana nao mimi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Sallallahu alaihi wasallam).
Rasulullah (sallallahu alaihi wasallam) akamwambia tena: “Baki hapa (pamoja nami).”
Swahaabi mwingine wakianswaar akasema: “Nitapigana nao mimi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (Sallallahu alaihi wasallam)
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Wewe nenda.” Swahabi huyu alipigana mpaka naye akauawa kishahidi.
Hili liliendelea kwa njia hii, huku kila mmoja kati ya maswahaabah kumi na mbili akisonga mbele, akipigana na kupata kifo cha kishahidi, mpaka tu Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na Talhah ibn Ubaydillah (Radhiyallahu ‘anhu) walibaki.
Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akasema tena: “Ni nani atakayepigana na watu hawa (na kututetea)?”
Talha (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema, “Nitakwenda kupigana nao.”
Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kisha akaendelea na kupigana kwa ushujaa na nguvu wa wale maswahaabah kumi na mmoja waliokuwa mbele yake mpaka mkono wake ukapigwa na adui, na vidole vyake vikakatika. Wakati huu, alionyesha uchungu wake na kusema, “Hiss!”
Baada ya hayo, Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) akamwambia: “Lau ungelitaja tu jina la Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’alah) (Wakati huo), Malaika wangeli kunyanyua kati ya watu na hali wao wangekutazama juu.” Wakati huo msaada wa Allah Ta’ala ulishuka na wa Mushrikeen wakaondolewa kutoka kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam) na Talhah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kupitia Malaika wanaomlinda Mtume (Sallallahu alaihi wasallam).
Katika hadith nyingine, imetajwa kwamba Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye alikuja kutangulia na pia akamlinda Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) kutokana na mashambulizi ya makafiri.