Fadhila Za Kuwatembelea Wagonjwa 2

Kuepushwa Mbali Na Moto Wa Jahannam Sawa Sawa Na Urefu wa Miaka Sabini

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Mwenye kufanya wudhu kamili (yaani. kwa kutimiza sunnah na vitendo vya mustahab vya wudhu) na akafunga safari kwenda kumtembelea ndugu yake Mwislamu mgonjwa kwa matumaini ya kupata thawabu za kumtembelea mgonjwa, mtu huyo atawekwa mbali urefu wa miaka sabini kutoka Jahannamu.”[1]

Kubaki Katika Bustani La Jannah

Thawbaan (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kumzuru ndugu yake Mwislamu (aliye mgonjwa) hubakia katika bustani la Jannah (tangu anapotoka) mpaka atakaporudi.”[2]

Kuzama Ndani Ya Rehma Ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)

Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Mtu anapokwenda kuwatembelea wagonjwa, anaingia katika rahmah ya Allah Ta’ala. Baada ya hapo, anapokaa na mgonjwa, anazama kabisa katika rahmah ya Allah Ta’ala.”[3]

Sifa Za Watu Wa Jannah

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba katika tukio moja, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliuliza kutoka kwa Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum), “Ni nani miongoni mwenu anafunga leo?” Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Mimi nimefunga leo.” Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza, “Ni nani miongoni mwenu ambaye amemtembelea mgonjwa leo?” Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) akajibu: “ Mimi nimemtembelea mgonjwa leo. Akauliza zaidi, “Ni nani kati yenu ambaye ameshiriki janazah leo?” Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Nimeshiriki katika janaazah leo.” Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza: “Ni nani kati yenu ambaye amemlisha masikini leo?” Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhu) akajibu, “Nimemlisha maskini leo.” Baada ya hapo, Mtume (SaSallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “Mwenye sifa zote hizi bila shaka ataingia Jannah.”[4]


[1] سنن الترمذي، الرقم: 2736، وقال: هذا حديث حسن

[2] صحيح مسلم، الرقم: 2568

[3] عن جابر بن عبد الله، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: من عاد مريضا لم يزل يخوض الرحمة حتى يجلس، فإذا جلس اغتمس فيها هذا حديث صحيح على شرط مسلم، ولم يخرجاه (المستدرك على الصحيحين للحاكم، الرقم: 1295، وقال العلامة الهيثمي – رحمه الله – في مجمع الزوائد 2/297: رواه أحمد والبزار ورجال أحمد رجال الصحيح

[4] صحيح مسلم، الرقم: 1028

About admin

Check Also

Fadhila Za Kutoa Salaam

Fadhila Ya Kutoa Salaam Wakwanza Abdullah bin Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (Sallallahu …