Wakati mmoja, ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alizungumza na mpwa wake ‘Urwah (rahimahullah) na akasema, “Ewe mpwa wangu! Baba zako wote wawili (baba yako na babu yako mzaa mama), Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), walikuwa miongoni mwa kundi la Maswahaba ambao Allah Ta’ala aliwazungumzia katika Aya ifuatayo kuhusiana na vita vya Uhud.
الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٢﴾
Ambao waliitikia wito wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) na Mtume, hata baada ya kuumizwa, kwa wale wamefanya mema miongoni mwao na kujiepusha na ubaya kwao ni malipo makubwa.
Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) akaendelea kusema: “Wakati ugumu ulipompata Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) siku ya Uhud (kutokana na makafiri kuwashambulia Waislamu na kumumiza Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) na makafiri walikuwa wameondoka, Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akaogopa wasije wakarejea (na kujaribu kuwashambulia Waislamu kwa mara nyingine). Kwa hivyo, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akatangaza, “Nani atawafuata (yaani makafiri)?”
Waliposikia tangazo hili, Maswahaabah sabini (Radhiya Allaahu ‘anhum) wa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) waliitikia wito na wakaenda kuwafuata makafiri. (Makafiri walikuwa na nia ya kurejea, lakini waliposikia kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ‘anhum) wamekuja kuwafuata, waliacha wazo lao la kurejea na wakakimbia). Miongoni mwa maswahaabah sabini alikuwemo Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) na Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu).” (Sahih Bukhaari #4077, Fat-hul Baari 7/432)