Kupata Dua Ya Malaika Elfu Sabini
Imepokewa kutoka kwa Ali (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kumtembelea mgonjwa asubuhi, Malaika elfu sabini humuombea rahma kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) mpaka jioni, na anayemtembelea mgonjwa jioni, Malaika elfu sabini humwomba rahma kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) mpaka asubuhi, na pia atapata bustani peponi.”
Kujenga Kasri Ndani Ya Jannah
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mtu anayemtembelea mgonjwa, Malaika wanaita kutoka mbinguni, ‘Baki katika raha na faraja. Ni vizuri kiasi gani kutembea kwako (kukutana na ndugu yako na kuonyesha kumjali) na (kupitia hatua hii,) umejijengea (mwenyewe) kasri katika Jannah.
Kupata Radhi Za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Siku ya Qiyaamah, Allah Ta’ala atasema, ‘Ewe mwana wa Aadam! Niliumwa, lakini haukunitembelea.’ Mtu huyo atajibu, ‘Ewe Allah Ta’ala, itawezekana vipi mimi nikutembelee Wewe unapoumwa na hali Wewe ni Mola wa ulimwengu wote? (yaani wewe si kama wanadamu wanaoumwa).’ Allah Ta’ala atajibu, ‘Je, hamjui kwamba mja wangu fulani aliumwa na haukumtembelea? Je, hujui kwamba kama ungemtembelea, bila shaka ungenikuta Mimi nipo?’”
[1] سنن الترمذي، الرقم: 969، وقال هذا حديث حسن غريب
[2] سنن ابن ماجة، الرقم: 1443، سنن الترمذي، الرقم: 2008، وقال: هذا حديث غريب
[3] صحيح مسلم، الرقم: 2569