Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) Akitoa Upanga Wake Kumlinda Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)

‘Urwah bin Zubair (rahimahullah) anasimulia yafuatayo:

Wakati mmoja, Shetani alizusha uwongo kwamba Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ametekwa na Makafiri katika eneo la juu la Makkah Mukarramah. Aliposikia uzushi huu, Zubair (Radhiyallahu ‘anhu), ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili tu wakati huo, mara moja akaondoka, akiwapita watu na upanga wake kumtafuta Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam). Wote waliomuona Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) walishangaa na kusema, “Yule kijana amebeba upanga!” Alipofika kwa Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam), Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akamuuliza: “Kuna nini ewe Zubair? Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamjibu kumfahamisha Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) kuhusu uzushi wa uwongo uliozushwa na akasema, “Nimekuja kuwapiga wale waliokukamata na upanga wangu.”

Katika riwaya nyingine, iliyopokelewa na mtoto wa ‘Urwah (rahimahullah), Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa mtu wa kwanza kuchomoa upanga wake kwa ajili ya Allah Ta‘ala. Riwaya hii inataja zaidi kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) aliposikia jibu hili la Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu), alimuombea du’aa.

Maelezo: Kuna riwaya tofauti kuhusiana na umri wa Zubair (Radhiyallahu ‘anhu) wakati wa kusilimu kwake. Kuna maoni mawili tofauti ambayo yamesimuliwa kutoka kwa ‘Urwah (rahimahullah). Abul Aswad anasimulia kutoka kwa ‘Urwah (rahimahullah) kwamba Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili aliposilimu, na Hisaam bin ‘Urwah (rahimahullah) anasimulia kutoka kwa baba yake, ‘Urwah (rahimahullah), kwamba alikuwa na umri wa miaka kumi na sita. Ama Hishaam bin ‘Urwah (rahimahullah), maoni yake ni kwamba Zubair (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na umri wa miaka kumi na tano aliposilimu. Pia kuna mtazamo wa Zubair (Radhiyallahu ‘anhu) akiwa na umri wa miaka minane wakati wa kusilimu. Alisilimu muda mfupi baada ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu). (Siyar A’laam min Nubalaa 3/27, Usdul Ghaabah 2/210, Musannaf ‘Abdur Razzaaq #9647, Musannaf ibn Abi Shaibah #19869)

About admin

Check Also

Uhuru wa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) na hamu ya Rasulullah (Sallallahu’ Alaihi Wasallam) kwa Bilaal (Radhiyallahu ‘Anhu) kuwa huru

Wakati mmoja, wakati akizungumza kuhusu Bilaal (Radhiyallahu 'Anhu), Sa'eed bin Musayyib (Rahimahullah) alisema:

Tamaa ya kuwa muisilamu ilikuwa kubwa sana moyoni mwa Bilal (Radi Allahu 'Anhu). Alikuwa akiwekwa chini na kuteswa katika mikono ya makafiri. Wakati wowote makafiri wangejaribu kumlazimisha kuachana na Uislamu, angekataa kwa nguvu na kutangaza waziwazi "Allah Allah" (yaani Allah Ta'ala ndiye mungu pekee anayestahili kuabudiwa).

Rasulullah (Sallallahu 'Alaihi Wasallam) kisha alikutana na Abu Bakr (Radhiyallahu' Anhu) na alionyesha hamu yake akisema, "Ikiwa tu tungekuwa na mali ambayo tunaweza kumnunua Bilaal (na kumwachisha huru)!" Baada ya hapo, Abu Bakr (Radhiyallahu 'Anhu) alimkaribia 'Abbaas (Radhiyallahu' Anhu) akamwambia, "Nenda umnunue Bilaal kwa niaba yangu."