Kuwatembelea Wagonjwa

Dini ya Uislamu inatetea na kuamrisha mtu kutimiza haki anazo daiwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) na haki anazo daiwa na waja wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Kuhusu haki anazodaiwa na waja wa Allah Ta’ala, hizi zinaweza kugawanywa katika aina mbili za haki.

Aina ya kwanza ni zile haki ambazo ni maalum kwa kila mtu k.m. haki ambazo mtu anazo daiwa na wazazi wake, ndugu, majirani, nk.

Aina ya pili ni zile haki zinazowahusu waislamu wote kwa ujumla. Kuhusiana na aina hii, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) ameeleza katika Hadithi kwamba kila Muislamu ana haki sita juu ya muislamu mwenzake. Miongoni mwa haki hizi sita mmoja kati yake ni mtu kumtembelea ndugu yake Mwislamu wakati anaumwa.

Ali (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Muislamu ana haki sita juu ya ndugu yake Muislamu. Akikutana naye amsalimie (kwa salaam); akimwalika basi akubali mwaliko wake; anapopiga chafya (na kusema alhamdulillah), ajibu chafya yake kwa kusema ‘Yarhamukallah’; mtu akiumwa basi amtembelee; mtu akifariki basi ahudhurie janaazah yake; na anapaswa kumpendelea ndugu yake kile anachojipendea yeye mwenyewe.”

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 7

17. Ni bora kuomba dua pana. Aaishah (radhiyallahu ‘anha) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …