21.Usiwe na haraka na kutokuwa na subra kwa ajili ya kukubaliwa na kutimizwa dua yako.
Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mja ataendelea kuwa katika hali ya wema maadamu yuko (ameridhishwa na amri ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) na hana haraka. MaSwahaabah wakauliza, “Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Kuwa na haraka kunamaanisha nini?” Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “Nilimwomba Mola wangu, lakini hakunijibu dua yangu.”
22.Ikiwa mtu anahisi kuwa dua zake hazikubaliwi, basi yeye asipoteze matumaini bali aendelee kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Anapaswa kuelewa kwamba Allah Ta’ala anajua lililo bora kwa kila mja na Allah Ta’ala atamruzuku
mja wake kwa mda muafaka.
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Khudri (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Muislamu yoyote akimuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), na haombi kitu cha haraam (yaani kuomba kitu chochote kisichoruhusiwa) au kukata uhusiano wakifamilia basi Allah Ta’ala atamjaalia moja kati ya mambo matatu. Ama atampa alichokuwa amekiomba (katika dunia hii), au atamwekea malipo ya dua yake katika aakherah, au atamuepusha na msiba kutoka kwake.” Maswahabah (radhiyallahu anhum) walisema, “Kama ni hivyo, sisi tutashiriki kwenye dua nyingi.” Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu: “Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) ndiye mjuzi ya kila kitu (yaani uwezo wake na hazina zake ni zaidi ya hayo mnayoyaomba).”
[1] مسند أحمد، الرقم: 13008، وقال العلامة المنذري رحمه الله في الترغيب والترهيب، الرقم: 2552: رواه أحمد واللفظ له وأبو يعلى ورواتها محتج بهم في الصحيح إلا أبا هلال الراسبي
[2] مسند أحمد، الرقم: 11133، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17210: رواه أحمد وأبو يعلى بنحوه والبزار والطبراني في الأوسط ورجال أحمد وأبي يعلى وأحد إسنادي البزار رجاله رجال الصحيح غير علي بن علي الرفاعي وهو ثقة