19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu kula haramu na kujihusisha na madhambi inazuia dua kujibiwa.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) ni Msafi na anakubali kilicho safi. Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) amewaamrisha waumini kwa amri ile ile aliyowapa Manabii (‘alaihimus salaam). (Kuhusu Manabii ‘alaihimus salaam) Allah Ta’ala amesema: “Enyi Mitume kuleni vilivyo safi na vyema na fanyeni vitendo vyema. Hakika mimi ninayajua yote mnayoyafanya.” (Kuhusu Waumini) Allah Ta’ala amesema: “Enyi Waumini, kuleni chakula vilivyo safi ambazo tuliowaruzukuni.” Baada ya hapo, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akaeleza hali ya mtu anayefanya safari ndefu yenye taabu. Nywele zake zimechafuka na mavazi yake yamefunikwa na vumbi. Anainua mikono yake mbinguni, huku akilia kwa kuomba, “Ewe Mola wangu, Ewe Mola wangu (Nisaidie katika shida)! Lakini, chakula chake na kinywaji ni haramu, nguo zake zinapatikana katika njia ya haramu. na mwili wake umelishwa kwa haramu, basi vipi dua zake zitakubaliwa?” (yaani, licha ya kuwa katika hali hii mbaya na ya kusikitisha, dua zake hazijibiwi).
20. Msiwalaani watoto zenu mnapoomba dua wakati wowote ile. Inawezekana kwamba laana yako inaweza kuendana na wakati ambapo dua zinakubaliwa.
Jaabir (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Msijilaani nafsi zenu, watoto zenu, watumwa wenu, wala mali zenu. Laana yako inaweza kuambatana na wakati (wa kukubalika) ambapo kikiombwa chochote kwa Allah Ta’ala kitakubaliwa.”
[1] صحيح مسلم، الرقم: 1015
[2]سنن أبي داود، الرقم: 1534، وقال العلامة المنذري رحمه الله مختصره 1/443: وأخرجه مسلم في أثناء حديث جابر الطويل