Maisha Ya Uislamu

Wakati mtu anazama na kujitahidi kuishi, atafanya chochote kuokoa maisha yake. Ikiwa ana uwezo wa kukamata kamba karibu na njia ambayo anaweza kujiondoa kutoka ndani ya maji, atashikamana nayo kwa bidii na kuiona kama njia yake ya kuokoa maisha yake.

Katika ulimwengu huu, muumini anapokabiliwa na mawimbi ya fitna ambayo inatishia kumzamisha katika madhambi na kuiharibu dini yake, basi anapaswa kujiuliza, “Ni njia gani ya Uislamu ninayopaswa kushikamana nayo kwa uthabiti?”

Njia ya Uislamu ni kuboresha uhusiano wa mtu na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Hili ndilo suluhu la matatizo yote, iwe yanahusiana na dini ya mtu au dunya.

Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alipohamia Madinah Munawwarah, kisha wakati wa Khutbah ya kwanza kabisa aliyoitoa, alihutubia watu akisema: “Mwenye kuboresha uhusiano wake na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) atamtosheleza kwa watu (yaani Allah Ta’ala atasimamia mambo yake na watu na kuboresha uhusiano wake nao).

Kuboresha uhusiano wa mtu na Allah Ta’ala ndio ufunguo wa kupata mafanikio katika dunia na akhera. Inaweza kulinganishwa na jua ambalo huangazia kila kitu duniani.

Mtu anapoangazia maisha yake kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) na kuboresha uhusiano wake na Muumba wake, basi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) humbariki kwa msaada wake na kumjaalia mafanikio katika kila kitu. Hata uhusiano wake na watu unaboreshwa na watu wanaanza kumpenda.

Hata hivyo, ili kuboresha uhusiano wa mtu na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), ni lazima kwa mtu kushikilia vipengele vitatu katika maisha yake.

Ya kwanza ni kushikamana na wakati wa Swalaah, ya pili ni kujiepusha na madhambi, na ya tatu ni kuonesha wema kwa viumbe, khususan familia ya mtu na jamaa.

Mshikamano Katika Swalaah

Swalaah imeelezwa katika Hadith kuwa ndio nguzo kuu ya dini ya mtu. Bila ya kushikamana na swalah, huwezi kuboresha uhusiano wako na Allah Ta’ala na kupata upendo na rehema Zake tukufu.

Ilikuwa ni matamanio ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa wanaume wa Ummah wake kuswali swala ya fardh pamoja na jamaa msikitini.

Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa na shauku kubwa ya kuswali pamoja na jamaa msikitini hadi hata katika ugonjwa wake uliokithiri kabla ya kufa kwake, alipokuwa hawezi kutembea bila kusaidiwa, alichukua msaada kwenye mabega ya watu wawili na akaenda msikitini kwa ajili ya kuswali.

Kuhusiana na wale wanaume waliokuwa wakiswali nyumbani kwao, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Lau si wanawake na watoto majumbani, ningeswali Ishaa na baada ya hapo ningeamuru kundi la vijana lichome moto nyumba za watu wanaoswali swalah zao za fard nyumbani kwao (bila udhuru yoyote halali).”

Katika Hadith ya Abdullah bin Mas’uud (radhiyallahu ‘anhu), imetajwa kwamba yule anayetaka kukutana na Allah Ta’ala Siku ya Qiyaamah akiwa Muislamu anatakiwa azichunge swala zake tano za kila siku kwa kuzitekeleza msikitini.

Kujiepusha Na Madhambi

Ili mtu aweze kuboresha uhusiano wake na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), ni wajibu kwake kujiepusha na madhambi na kujilinda mwenyewe kutokana na fitnah zote.

Muhadith mkubwa, Allaamah Yusuf Binnowri (rahimahullah), ametaja, “Katika kila zama, fitna zinajidhihirisha kwa namna tofauti. Hata hivyo, kimsingi, kuna aina mbili za fitna zinazodhuru dini ya mtu; fitnah katika amal (vitendo) na fitnah katika ilm (elimu).”

Allaamah Binnowri (rahimahullah) baada ya hapo akaeleza kwamba fitnah katika amal hutokea pale watu wanapojihusisha na madhambi kama vile mahusiano waki na haramu, zinaa, unywaji wa pombe na madawa ya kulevya, riba, rushwa, kua bila hayaa, kuvaa uchi, kucheza mziki, kuimba muziki.

Dhambi hizi humpelekea mtu kujiingiza katika dhuluma, kusema uwongo, kutokuwa mwaminifu katika biashara, nk.

Madhara ya dhambi hizi mwishoni huathiri Swalaah ya mtu, Saumu, Zakaah, Hajj na matendo mengine yote ya haki. Jinsi mtu anajiingiza zaidi katika madhambi haya na kuzama ndani yake, basi dini yake inakuwa dhaifu, na mtu pole pole atapoteza taufiq ya kutekeleza matendo mema.

Kuhusu fitna ya ilm (elimu), basi hii inakuja kwa mtu ambaye anatafuta dini yake kutoka vyanzo visivyotegemewa na visivyo vya Kiislamu (k.m. TV, Youtube, Facebook, n.k.).

Mtu kupata dini yake kutoka kwa vyanzo hivi vya ufisadi, moyo wake na akili vitaumbwa ipasavyo, na kumfanya awe na
uelewa mbaya katika mtazamo wa deen. Kwa hivyo, matendo atakayoyafanya baada ya hapo yataendana na mawazo ambayo ameyapata kutoka kwenye vyanzo hivi.

About admin

Check Also

Allah Ta’ala – Anaye Ruzuku Viumbe Vyote

Wakati mmoja, kipindi cha Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), kundi la Maswahabah (radhiyallahu anhum) kutoka kabila …