Utabiri Wa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kuhusiana na Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) Kushinda Qaadisiyyah

Katika tukio la Hajjatul Wadaa’, Sa’d (Radhiyallahu ‘anhu) alikuwa ameumwa huko Makka Mukarramah na alihofia kwamba angeaga dunia. Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuja kumtembelea, alianza kulia. Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akamuuliza: “Kwa nini unalia?” Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu, “Nahofia kuwa nitafariki katika ardhi ambayo niliifanya Hijrah, na kwa kufariki hapa, malipo ya hijrah yangu yatapotea.”

Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) kisha akaomba du’aa ifuatayo mara tatu kwa ajili ya Sa’d (Radhiyallahu ‘anhu) kupona, “Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Mponye Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu)!”

Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) baada ya hapo akamuuliza Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam)! Nina mali nyingi, na nina binti tu ambaye yuko kwenye maisha mazuri. Je, ninaweza kufanya wasiyya kwa mali yangu yote (itolewe sadaka baada ya kufa kwangu)?” Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu, “Hapana.”

Kisha Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) akauliza, “Je, ninaweza kutoa wasiyya ya theluthi mbili ya mali yangu (itolewe sadaka baada ya kufa kwangu)?” Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu, “Hapana.”

Kisha Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) akauliza kama angeweza kuomba nusu ya mali yake kutolewa katika sadaka baada ya kufariki kwake, ambapo Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alijibu kwa kukanusha.

Mwisho, Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuliza Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) kama angeweza kuomba theluthi moja ya mali yake itolewe sadaka baada ya kufariki kwake. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu: “(Ndio unaweza kuusia) thuluthi, lakini kuusia thuluthi ni nyingi). Hakika sadaka yote unayotoa katika mali yako ni sadaka, na chochote unachotoa kwa wanaokutegemea ni sadaka, na chochote anachotumia mkeo katika mali yako ni sadaka, na kwako wewe kuwaacha familia yako wakiwa vizuri kifedha (baada ya kufariki kwako) ni bora kuliko kuwaacha (katika hali yaumaskini) wakinyoosha mikono yao mbele ya watu (wanaoomba kwa sababu ya umaskini).”

Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) baada ya hapo akamwambia Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) akisema, “Hakika wewe utabaki hai, mpaka watu wengi watafaidike kupitia wewe, na wengine wengi watadhurika kupitia wewe.” (Sahih Muslim #1628)

Baadhi ya Muhadditheen wanasema bashara hii ya Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ilikuwa inamrejelea Sa’d (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuiteka ardhi ya Qaadisiyyah ambayo Waislamu walinufaika na madhara yakawafikia makafiri.

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …