Sunna Na Adabu Za Dua 4

9. Wakati wa kuomba dua, moyo wako unapaswa kulenga kikamilifu na
makini kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Moyo wako usiwe umeghafilika na kutojali wakati wa omba dua. Hupaswi kuangalia huku na huku na kuwangalia watu pindi unapoomba dua.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Muombeni Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kwa yakini ya kujibiwa dua yako, na kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) hajibu dua inayotoka kwenye moyo ulioghafilika na usiojali.”

10. Muombe Allah (Subhaanahu Wata’aala) mahitaji yako yote, yakiwa makubwa au madogo.

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Kila mmoja wenu arejee kwa Mola wake Allah Ta’ala kwa ajili ya haja yake au kwa mahitaji yake yote (msimulizi alitoa shaka ya kwamba neno la Hadith lilikuwa ni kwa ajili ya haja yake” au ‘ kwa mahitaji yake yote’), kiasi kwamba anapaswa pia kumuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kamba ya kiatu chake kinapokatika, au hata kumwomba chumvi (anapohitaji chumvi).”

11. Usifanye dua tu wakati unapofikiwa na matatizo. Bali fanya dua kila wakati, iwe katika shida au mafanikio.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kutaka Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) amjibu dua zake wakati wa shida, basi anapaswa kuomba dua nyingi wakati wa raha na faraja.”

About admin

Check Also

Sunnat Na Adabu Za Kuamkiana (Kutoa Salaam) 7

26. Ni adabu kwamba mtu anapotembea na mwingine amekaa, basi anayetembea aanze kutoa salamu wa …