Khutba Ya Kwanza Huko Madina Munawwarah baada ya Hijrah

Katika tukio la hijra, wakati Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipoingia kwenye mji uliobarikiwa wa Madinah Munawwarah, watu wengi walikuwa wakimgojea kwa hamu.

Miongoni mwao walikuwemo wale wanaompenda Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) -Ansaar wa Madinah Munawwarah – pamoja na Mayahudi na wale wanao abudu masanamu waliokuwa wakiishi katika mji huo.

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alitoa khutba ya mbele ya kilamtu ambamo aliwaalika watu kwenye mafundisho mazuri ya Uislamu. Wasiokuwa Waislamu walikuwa na shauku kubwa ya kukutana na mtu aliyedai utume na kusikia ujumbe wake, na hivyo wengi wao walikuja kusikiliza khutba yake.

Abdullah bin Salaam (radhiyallahu ‘anhu) Akisilimu

Abdullah bin Salaam (radhiyallahu ‘anhu), ambaye alikuwa kama sheikh wa kiyahudi wakati huo, anaelezea kukutana kwake kwa mara ya kwanza na Mtume wa Mwenyezi Mungu (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa maneno yafuatayo:

“Nilikuwa miongoni mwa watu waliokuja kumuona Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), na macho yangu yalipoangukia kwenye uso wake uliobarikiwa, mara moja nilijua kwamba uso wake haukuwa uso wa muongo.

“Maneno ya kwanza kabisa yaliyotoka katika kinywa chake kilichobarikiwa yalikuwa, ‘Enyi Watu! Ifanye salaam kuwa desturi ya kawaida miongoni mwenu, wapeni watu chakula, jiungeni na familia zenu, na simamisheni Swalaah ya usiku pindi watu wamelala, mtaingia Jannah kwa salaam (kwa amani na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala).’”

Huu ulikuwa ni hisia ya kwanza iliyoachwa ndani ya moyo wa Abdullah bin Salaam (radhiyallahu ‘anhu) na wengine kuhusu uzuri wa Uislamu.

Aliona kuwa Uislamu ni dini ambayo haitetei haki tu, bali inakwenda mbali zaidi katika kukuza huruma na wema wakati wa kuwa na viumbe. Ilikuwa ni kwa ajili ya hili kwamba baadaye Abdullah bin Salaam (radhiyallahu ‘anhu) alisilimu.

Wema Na Upendo Katika Kila Upande Wa Maisha

Tunapofikiria kuonyesha wema na upendo kwa viumbe, basi kawaida kazi za ihsani na sadaka huja akilini. Lakini, kuonyesha wema na upendo kwa viumbe haija wekewa mipaka katika hili. Badala yake, wema na upendo vinapaswa kupatikana katika kila nyanja ya
maisha ya Muislamu.

Liwe neno la kumtia moyo mtu aliyekandamizwa, kutoa nasaha kwa aliye na shida, kuwapa chakula masikini, kuwafariji waliofiwa, kuwasaidia walio na shida za kifedha, kumsalimia Muislamu pembeni yako kwa tabasamu na kuleta furaha moyoni mwake, jitihada za kujiepusha na kusababisha maumivu na usumbufu wowote kwa watu, wawe Waislamu au wasiokuwa Waislamu, na kupuuza makosa ya watu – yote haya ni tafakari ya roho ya wema na upendo ambayo ilionyeshwa na kipenzi chetu Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuwa akishughulikia viumbe katika maisha yake yote.

Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) atujaalie uwezo wa kumuiga Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) katika nyanja zote za maisha yetu na atujaalie uzuri wa Uislamu ili kila tuendako tuangaze maadili ya kweli ya Sunna na kuwa mwaliko kwa makafiri kusilimu.

About admin

Check Also

Allah Ta’ala – Anaye Ruzuku Viumbe Vyote

Wakati mmoja, kipindi cha Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), kundi la Maswahabah (radhiyallahu anhum) kutoka kabila …