Sunna Na Adabu Za Dua 5

12. Baada ya kumaliza dua yako, sema aameen.

Abu Musabbih Al-Maqraaiy anasimulia: Wakati mmoja, tulikuwa tumekaa na Abu Zuhair An-Numairi ambaye alikuwa miongoni mwa maswahaabah (radhiyallahu anhum). Alikuwa mfasaha zaidi katika lugha. Wakati mtu yoyote miongoni mwetu alikuwa akishiriki katika dua, alikuwa akisema: “ufunge dua hiyo kwa Aamin, kwa sababu Aamin ni kama muhuri kwenye karatasi.” Kisha akasema zaidi, “Je, nisikujulisheni kuhusu hili? Usiku mmoja, tulitoka pamoja na Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) na tukakutana na mtu ambaye alikuwa akishiriki kwenye dua. Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akasimama kumsikiliza na akasema: ‘Ikiwa atafunga dua yake, basi ataufanya Jannah uwe laazim kwake.” Mmoja kati yetu akauliza: “Vipi ataifunga (Dua yake)?” Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu: afunge dua yake na aamin? Akiufunga dua yake na Aamin, basi ameifanya Jannah kuwa faradhi kwake.” Yule ambaye alimuuliza Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akamwendea mtu huyo na kusema: “Ewe fulani na fulani, malizia dua yako kwa kusema Aamin na itikia bashara (ya Mtume sallallahu ‘alaihi wasallam).’”

13. Baada ya kumaliza dua yako, msalie Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam).

Umar (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia, “Dua inabaki kusimamishwa kati ya mbingu na ardhi. Haifiki mbinguni mpaka salaa na salaam isomwe juu ya Nabi (sallallahu ‘alaihi wasallam) (yaani hakuna dhamana ya kukubaliwa kwao).”

14. Baada ya kumaliza dua, pitisha viganja vyako juu ya uso wako.

Umar (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba wakati wowote Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akiinua mikono yake kwenye dua, yalikuwa hayashuki mpaka aifute juu ya uso wake.

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 7

17. Ni bora kuomba dua pana. Aaishah (radhiyallahu ‘anha) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …