Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) Akimlinda Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)

‘Aaishah (radhiya allaahu ‘anha) anasimulia:

Baada ya hajiria Madinah Munawwarah, katika tukio moja, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) hakupata usingizi usiku (kwa kuhofia kwamba maadui wangemshambulia). Hapo ndipo Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliposema: “Laiti kungekuwa na mchamungu wa kunilinda usiku huu.” Tukiwa katika hali hiyo, tulisikia milio ya silaha. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akauliza, “Nani yupo?” Mtu huyo akajibu, “Sa’d bin Abi Waqqaas (radhiya allaahu ‘anhu).” Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akamuuliza: “Ni nini kimekuleta hapa?” Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu: “Nilihofia maisha yako, ewe Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), na kwa hivyo nimekuja kukulinda. Aliposikia hivyo, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alimuombea du’a kisha akalala. (Sunan Tirmizi #3756, Fat-hul Baari 6/96)

Katika riwaya nyingine, ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ametaja kuwa Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) atalindwa na Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) mpaka ikateremshwa aya ifuatayo ya Qur’an Takatifu:

وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ

Na Allah Ta’ala atakulinda na (madhara ya) watu

Ilipoteremka Aya hii ya Qur’an Takatifu, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwataja Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum), “Enyi watu! Ondokeni, kwa sababu Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) amenipa ulinzi wake takatifu.” (Sunan Tirmizi #3046)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …