binary comment

Sunna Na Adabu Za Dua 3

6. Unapo omba dua, usitumi njia ya kutokuwa na uhakika. Kwa mfano, usiseme: “Ewe Mwenyezi Mungu, ukitaka kunitimizia haja yangu, basi unitimizie.”

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “(Wakati wa kuomba dua) mtu asiseme ‘Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, nipe rizki ukitaka. Muombe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kwa huruma na kwa kujiamini (kwamba Allah Ta’ala Atamtimizia haja zake. Mtu asimuombe Allah Ta’ala ampe fadhila zake akipenda) kwa sababu Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Hufanya Apendavyo, hakuna wa kumlazimisha (kufanya lolote).

7. Kuwa na matumaini kamili katika rehma ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) huku ukiomba dua. Omba dua na imani kwamba dua yako itajibiwa.

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Muombeni Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) na imani na yakini ya kujibiwa dua yako, na kumbuka kwamba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) hajibu dua iliotoka kwenye moyo ya kutokujali.”

8. Moyo wako na matumaini yako yaelekezwe kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) peke yake. Msitegemee chochote kwa mtu mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Usifikiri kwamba kupitia mtu fulani au jambo fulani, hitaji lako litatimizwa.

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …