Du’aa Maalum Ya Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam):

‘Aaishah binti Sa’d (radhiya allaahu ‘anha), binti wa Sa’d (radhiya Allaahu ‘anhu) ‘anhu), anasimulia yafuatayo kutoka kwa baba yake, Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu):

Wakati wa Vita vya Uhud, (wakati maadui waliposhambulia kutoka nyuma na Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) wengi wakauawa kwenye uwanja wa vita,) Maswahabah (radhiya allaahu ‘anhum) hawakuweza kumpata Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa. Wakati huo, nilikwenda pembeni na kujisemea, “Nitaendelea kupigana na makafiri. Katika harakati za kupigana, ama nitapata kifo cha kishahidi au Allah Ta’ala ataniruhusu kubaki hai. Nikinusurika katika hii vita, basi hakika, nitakutana na Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam).”

Nikiwa katika hali hii, ghafla nilimuona mtu akiwa amejifunika uso wake kwa sababu sikuweza kumtambua. Makafiri wakasogea mbele mpaka nikasema moyoni: Wamemfuata mpaka wakamfikia! Wakati huo, mtu huyo alijaza kokoto mkononi mwake na akawatupia kwenye nyuso za makafiri, na wakageuka na kurudi nyuma mpaka wakafika mlimani. Mtu huyo alirudia kitendo hiki mara nyingi (wakati makafiri walipojaribu kumshambulia), na sikujua alikuwa nani (kwa sababu sikuweza kuuona uso wake).

Baina yangu na mtu huyu alikuwa Miqdaad bin Aswad (radhiya allaahu ‘anhu). Nilikuwa nimeamua tu kumuuliza Miqdaad (radhiyallahu ‘anhu) ni nani mtu huyu mkubwa pale Miqdaad (Radhiyallahu ‘anhu) aliponiambia, “Ewe Sa’d (radhiyallahu ‘anhu)! Huyu ni Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) ambaye anakuita!” Nilimuuliza Miqdaad (radhiya allaahu ‘anhu), “Yuko wapi Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)?” Kwa kujibu, Miqdaad (radhiyallahu ‘anhu) aliashiria kwa mtu yule yule.

Kwa kutambua kwamba mtu huyu hakuwa mwingine bali ni Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kipenzi cha Allah Ta‘ala, mara moja nilisimama, na kwa ajili ya furaha iliyopitiliza, nilisahau kabisa na kuto hisi majeraha na maumivu yoyote. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia, “Ewe Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu)! Umekuwa wapi muda wote huu?” Nilimjibu nikisema, “Nilikuwa nimesimama kwa mbali kutoka kwako, kutoka mahali nilipoweza kukuona (mpaka adui aliposhambulia na nikakupoteza).”

Kisha Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akanikalisha mbele yake na nikaanza kurusha mishale kuwaelekea makafiri huku nikisema, “Ewe Mwenyezi Mungu! Huu ni mshale wako, kwa hiyo uufanye uwapige maadui zako!” Nilipokuwa nikirusha mishale, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akiniombea du’aa akisema: “Ewe Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)! Jibu du‘aa ya Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu)! Ewe Mwenyezi Mungu! Ifanye mishale ya Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) ipige mahali pake!” Kisha Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akaniambia, “Endelea kurusha mishale, ewe Sa’d! Baba yangu na mama yangu watolewe kafara kwa ajili yako!” Sikurusha mshale hata mmoja isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliendelea kuomba dua kwa Allah Ta’ala ili kuupiga mshale wangu na uwafikie makafiri na kujibu dua yangu ninapomuomba.

Hatimaye, mishale yote kwenye podo langu ilipokwisha, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alitandaza mishale ya podo lake na kunikabidhi mshale wenye manyoya juu yake nipige katika njia ya Allah Ta’ala.

Imaam Zuhri (rahimahullah) ametaja kwamba Sa’d (radhiyallahu ‘anhu) alirusha mishale 1000 katika Vita vya Uhud. (Mustadrak Haakim #4314)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …