Ndoto Ya Sa’d (radhiyallahu ‘anhu) Kabla ya Kusilimu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) anasimulia kwamba:

Kabla ya kusilimu, niliota ndoto ambayo niliona niko gizani kabisa na kutokuona chochote. Ghafla, mwezi ukatokea ambalo ulianza kumulika usiku. Kisha nikaufuata huo mwanga hadi nikaufikia mwezi. Katika ndoto, niliona watu fulani ambao walikuwa wamenitangulia kuufikia mwezi. Nilimuona Zaid bin Haarithah, ‘Ali bin Abi Taalib na Abu Bakr (radhiya allaahu ‘anhum) wakiwa karibu na mwezi. Nikawauliza, “Ni lini nyinyi mlifika hapa (kwenye mwezi)?” Wakajibu, “Tumefika hapa sasa hivi.”

Nilipoamka kutoka kwenye ndoto hiyo, niligundua kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akitangaza nubuwwah na alikuwa analingania Uislamu kwa siri. Hivyo nilimwendea na kukutana naye kwenye mabonde ya Makkah Mukarramah. Nilipofika pale nilikuta amemaliza kuswali. Kisha nikasilimu mikononi mwake. Zaidi ya hawa maswahaabah (Zaid bin Haarithah, ‘Ali bin Abi Taalib na Abu Bakr radhiyallahu ‘anhum), hakuna mtu mwingine yoyote aliyesilimu kabla yangu.

Maelezo:

1. Giza kwenye ndoto ya Sa’d (radhiyallahu anhu) lilimaanisha giza la ukafiri. Mwezi wenye nuru ulikuwa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) ambaye alitumwa na nuru ya Uislamu kuondoa giza duniani.

2. Sa’d (radhiyallahu anhu) ametaja kuwa mbali na Zaid bin Haarithah, Ali bin Abi Taalib na Abu Bakr (radhiyallahu ‘anhum), hakuna mtu mwingine yoyote aliyesilimu kabla yake. Lakini, hii ilikuwa kulingana na ufahamu wake. Kwa sababu katika riwaya zingine, inathibitika kwamba kulikuwa na Maswahaabah wengine wachache waliosilimu kabla yake). (Usdul Ghaabah 2\309)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …