Nyakati Ambapo Dua Zinakubaliwa

Wakati wa Adhaan na Wakati Majeshi Mawili Yanapokutana Katika Vita

Sahl bin Sa’d (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Kuna nyakati mbili ambazo dua hazikataliwi au mara chache sana dua zinazo ombwa katika nyakati hizi mbili hazitakubaliwa; wakati wa adhaan na wakati majeshi mawili yanapokutana vitani.”[1]

Kati Ya Adhaan na Iqaamah

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Dua inayo ombwa kati ya adhaan na iqaamah haikataliwi.”[2]

Katikati Ya Usiku

Uthmaan bin Abil Aas Thaqafi (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Milango ya mbingu inafunguliwa inapopita nusu ya usiku. Kisha Malaika anaita, ‘Je, kuna yoyote anayeomba dua ili dua yake ikubaliwe? Je, kuna yoyote anayeomba chochote ili ombi lake likubaliwe? Je, kuna mwenye shida ili kupunguziwa dhiki yake?’ Baada ya hapo, hakuna Muislamu yoyote anayeomba dua kwa Allah Ta’ala isipokuwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Anajibu dua yake, isipokuwa kahaba au mtu anayepora mali za watu kwa nguvu. ”[3]

Dua baada Ya Swalaah Ya Fardh na Wakati wa Tahajjud

Abu Umaamah (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba katika tukio moja, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliulizwa, “Ni dua gani inayosikika zaidi (na kukubalika kwa urahisi)?” Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu: “Dua inayo ombwa katika sehemu ya mwisho ya usiku na baada ya Swalaah ya fardh.”[4]


[1] سنن أبي داود، الرقم: 2540، وسكت عنه هو والمنذري في مختصره

[2] سنن أبي داود، الرقم: 521، سنن الترمذي، الرقم: 212، وقال: حديث أنس حديث حسن

[3] المعجم الكبير للطبراني، الرقم: 8391، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17245: رواه الطبراني ورجاله رجال الصحيح

[4] سنن الترمذي، الرقم: 3499، وقال هذا حديث حسن

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …