Rizki Ipo Mikononi Wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Peke Yake

Kila kiumbe anahitaji rizki kwa ajili ya kuendelea kwake na kuishi kwake, na rizki iko mikononi mwa Allah Ta’ala peke yake.

Sifa, nguvu na akili sio msingi kuamua rizki ya mtu. Ni kweli jinsi maneno ya mshairi alikuwa akisema:

ينال الفتى من عيشه وهو جاهل ويكدى الفتى في دهره وهو عالم
ولو كانت الأرزاق تجرى على الحجى هلكن إذا من جهلهن البهائم

Mtu hupata rizki (kwa wingi) licha ya yeye kutokuwa na akili. Mtu mwingine anaachwa kuwa maskini, licha ya yeye kuwa na elimu na akili.

Lau ugawaji wa rizki ungeegemezwa kwenye akili, basi wanyama kwa sababu ya ujinga wao, wangeangamia wote.

Kumtegemea Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)

Katika Hadith, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliuusia ummah akisema: “Mkiwa na tawakkul na kumtegemea Allah Ta’ala jinsi mnavyopaswa, basi Allah Ta’ala atakupeni riziki kama anavyowaruzuku ndege. Ndege huondoka kwenye viota vyao asubuhi na mapema wakiwa na njaa, na hurudi jioni wakiwa wameshiba tumboni.”

Kujiepusha Na Haraam

Kuwa na tawakkul na kumtegemea Allah Ta’ala ndio ufunguo wa kupata mafanikio katika maisha ya mtu na pia njia ya kupata baraka katika riziki ya mtu. Lakini, kumtegemea Allah Ta’ala vile vile kunahusisha mtu kufuata njia halali ili apate riziki na kuhakikisha kwamba mtu havunji maamrisho ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) wakati wowote.

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Enyi watu! Mcheni Allah Ta’ala na fanyeni juhudi ya kawaida katika kutafuta riziki ya halali. Na yoyote miongoni mwenu akiona riziki yake imecheleweshwa basi asiitafute kwa njia ambayo atamuasi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), kwa sababu hakika neema ya Allah Ta’ala haiwezi kupatikana kwa kujihusisha na madhambi.

Tukio la Nabi Musa (‘alaihis salaam) Na Mdudu

Imeripotiwa kwamba wakati Nabi Musa (alaihis salaam) alipopokea utume na kuamrishwa na Allah Ta’ala kuwaita watu kwenye Uislamu, alikuwa na wasiwasi na mawazo ya jinsi gani atatunza familia yake.

Hapo hapo, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Akamwamrisha Nabi Musa (alaihis salaam) kupiga jiwe fulani kwa kutumia fimbo lake. Alipoupiga ule mwamba, alikuta mwamba huo umepasuka, na ndani yake kulikuwa na mwamba mwingine.

Nabi Musa (alaihis salaam) ndipo alipoamrishwa kupiga mwamba wa pili. Alipoupiga, alikuta ndani yake kulikuwa na mwamba wa tatu.

Wakati Nabii Musa (alaihis salaam) alipiga mwamba wa tatu na fimbo lake, lilipasuka, na kufichua mdudu mdogo ndani. Mdudu huyu mdogo alikuwa amefichwa chini ya tabaka tatu za miamba, iliyofichwa machoni mwa watu wote na dunia, lakini ilikuwa inakula rizki yake iliyoruzukiwa na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)

Kisha Allah Ta’ala akamruhusu Nabii Musa (alaihis salaam) kusikia maneno ya mdudu huyo huku ikimsifu Allah Ta’ala. Mdudu huyo alikuwa akimtukuza Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kwa maneno yafuatayo:

سبحان من يراني ويسمع كلامي ويعرف مكاني ويذكرني ولا ينساني

Ametakasika Mwenye kuniona, na anasikia maneno yangu, na anajua kwenye nilipo, na ananikumbuka na wala hanisahau.

Aliposikia maneno ya mdudu huyo akimtukuza Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), Nabii Musa (alaihis salaam) akatambua kwamba Allah Ta’ala alitaka kumuonyesha kwamba yeye ndiye anayeruzuku kila kiumbe hata mdudu mdogo kabisa, na hivyo Allah Ta’ala atamruzuku yeye na familia yake

About admin

Check Also

Sifa Ya Amaanah – Fikra Ya Kuulizwa

Allah Ta’ala amemneemesha mwanadamu kwa neema zisizohesabika. Baadhi ni neema za kimwili, wakati nyingine ni …