Watu Ambao Dua Zao Zinakubaliwa

Mtu Mgonjwa

Umar (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Unapokutana na mgonjwa basi muombe akuombee dua, kwa sababu dua yake ni kama dua ya Malaika (yaani kwa ajili ya ugonjwa huo madhambi zake yamesamehewa, kwa hiyo anafanana na Malaika kwa kutokuwa na madhambi, na ndo maana dua yake itakubaliwa haraka).”[1]

Anayeomba Dua Kipindi Cha Raha na Faraja

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Mwenye kutaka Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) amjibu dua zake wakati wa shida na taabu, basi aombe dua nyingi kipindi cha raha na faraja.”[2]

Yule Anayemsaidia Mtu Katika Ugumu Wa Kifedha

Ibnu Umar (radhiyallahu anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Mwenye kutaka kujibiwa dua yake, na matatizo yake yapunguzwe, amsaidie mtu katika matatizo ya kifedha.”[3]

Mzee Mwenye Nywele Nyeupe

Imepokewa kutoka kwa Anas (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Hakika Allah Ta’ala anaona haya kukataa dua ya mtu (mzee) mwenye nywele nyeupe, wakati ameongoka na amesimama imara kwenye sunnah.”[4]

Mtu Anayeomba Dua Kwenye Mkusanyiko

Imepokewa kutoka kwa Habib bin Maslamah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Hakuna kundi la watu linalokusanyika, kisha baadhi yao wanaomba dua na wengine wanasema “Amin, isipokuwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) anakubali dua zao.”[5]


[1] سنن ابن ماجه، الرقم: 1441، وقال العلامة البوصيري رحمه الله في مصباح الزجاجة (2/21): هذا إسناد رجاله ثقات إلا أنه منقطع قال العلائي في المراسيل والمزي في التهذيب أن رواية ميمون بن مهران عن عمر مرسلة

[2] سنن الترمذي، الرقم: 3382، وقال: هذا حديث غريب

[3] مسند أحمد، الرقم: 4749، ورجال أحمد ثقات كما في مجمع الزوائد 4/133

[4] المعجم الأوسط للطبراني، الرقم: 5286، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17213: وفيه صالح بن راشد وثقه ابن حبان وفيه ضعف وبقية رجاله ثقات

[5] المستدرك على الصحيحين للحاكم، الرقم: 5478، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17347: ورجاله رجال الصحيح غير ابن لهيعة وهو حسن الحديث

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …