Imani Madhubuti Ya Ali (radhiya allaahu ‘anhu) katika Ahadi ya Allah Ta’ala

Imepokewa kwamba siku moja, ombaomba mmoja alikuja kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) na kuomba kitu. Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alimgeukia mmoja wa wanawe wawili, ima Hasan au Husein (radhiya allaahu ‘anhuma), na akamwambia, “Nenda kwa mama yako na umwambie kwamba nilisema, ‘Nilihifadhi dirham sita kwako, basi nipe dirhamu moja katika zile sita (ili nimpe mwombaji).

Mtoto alikwenda kwa mama yake, Faatimah (radhiyallahu ‘anha), na baada ya hapo akarudi na ujumbe ifuatayo. Akamwambia baba yake, “Mama yangu alisema kwamba ulimwekesha dirham sita kwa ajili ya kununua unga.” Aliposikia hivyo, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alisema: “Imaan ya mja haitakuwa mkweli na mkamilifu mpaka ategemee zaidi yale ambayo yamo mikononi mwa Allah Ta’ala kuliko yale yamo mikononi mwa mtu (yaani mja amtegemee Allah Ta’ala na ahadi Zake kwa kutoa sadaka atabarikiwa na baraka nyingi kwa jambo jema na asizuie mali yake kwa kuhofia umasikini).

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akamwambia mwanawe, “Nenda kwa mama yako na mwambie anipe dirham sita zote (ili nimpe mwombaji).” Hivyo alikwenda kwa mama yake na kisha akarejea na dirham sita ambazo Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimkabidhi yule mwombaji.

Muda mfupi baadaye, mtu mmoja alipita kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akiwa na ngamia ambaye alikuwa akiuza. Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akamuuliza, “Unauza ngamia kwa bei gani?” Yule mtu akajibu, “Ninaiuza kwa dirham mia moja na arobaini.” Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akamnunua ngamia kutoka kwake. Baada ya kumnunua ngamia, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alisema: “Mfunge ngamia hapa, na tutakulipa baadaye.” Yule mtu akamfunga ngamia na kuondoka zake.

Baadaye, mtu mwingine akapita, na alipomwona ngamia, akauliza, “Huyu ngamia ni wa nani? Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu, “Ni wa kwangu.” Mwanamume huyo akauliza, “Je, unaiuza?” Wakati Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alipomjibu kwamba anaiuza, mtu huyo aliuliza, “Unaiuza kwa bei gani?” Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akamjibu, “Ninaiuza kwa dirham mia mbili.” Mwanamume huyo aliridhika na bei hiyo na hivyo akakubali ombi hilo na wakamalizana kwa kusema, “Nimeinunua kwako.” Kisha akatoa dirham mia mbili na kuumpa Ali (radhiya allaahu ‘anhu), akamchukua ngamia wake na akaondoka.

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akaenda kwa yule mtu aliyemuuzia ngamia na kumlipa dirham mia na arobaini alizokuwa akidaiwa. Baada ya hapo, alirudi nyumbani kwa mke wake mheshimiwa, Faatimah (radhiyallahu ‘anha), akiwa na dirham sitini alizozipata kama faida (na akampa).

Pindi Faatimah (radhiya allaahu ‘anha) alipoziona dirham sitini, alimuuliza, “Hii ni nini? Pesa hizi zimetoka wapi?” Ali (radhiya allaahu ‘anhu) akajibu: “Haya ndiyo aliyotuahidi Allaah (Ta’ala) kupitia maneno yafuatayo yameteremshwa kwenye ulimi uliobarikiwa wa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam).”

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akasoma aya ifuatayo ya Qur-aan Takatifu:

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا

Mwenye kuleta kheri moja atapata ujira mara kumi (kwa kitendo alichokifanya) (An’aam Aya:160)

Kwa maneno mengine, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alimueleza Faatimah (radhiya allaahu ‘anha) kwamba alipotumia dirham sita katika sadaqah, Allah Ta’ala alimbariki kwa malipo mara kumi zaidi ya yale aliyotoa, na hivyo sasa alikuwa na dirhamu sitini badala ya dirhamu sita alizozitoa na kuumpa ombaomba. (Hayaat-us-Sahaabah 2/191) 

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …