Watu Ambao Dua Zao Zinakubaliwa

Wazazi, Wasafiri na Wenye Kudhulumiwa

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Dua tatu ni kwamba bila shaka zitakubaliwa; Dua ya baba (au mama kwa mtoto wao), Dua ya musaafir (msafiri) na dua ya mwenye kudhulumiwa.”[1]

Mwenye Kufunga Na Imaamu Muadilifu

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema: “Watu watatu ni kwamba dua zao hazitakataliwa; mwenye kufunga mpaka afungue saumu yake, imaamu muadilifu, na dua ya mwenye kudhulumiwa ambayo Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) ataiinua juu ya mawingu, na milango ya mbingu zitafunguliwa, na Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Atasema, ‘Kwa utukufu wangu! Hakika nitakusaidia – hata ikiwa ni baada ya muda fulani!’”[2]

Mwenye Kumfanyia Dua Ndugu Yake Muislamu haliyakuwa hayupo

Abdullah bin Amr bin aas (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema: “Hakika dua inayokubaliwa kwa haraka zaidi ni dua ambayo mtu humfanyia mtu wakati hayupo.”[3]

Mujaahid Na Mwenye Kuhiji Au Mwenye Kufanya Umra

Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu) amesimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Mujaahid na wale wanaohiji na wale wanaofanya umrah ni wakilishi wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Wakimuomba Allah Ta’ala, basi huwajibu dua zao, na wakimwomba chochote huwapa.”[4]


[1] سنن الترمذي، الرقم: 3448، وقال: هذا حديث حسن

ولم يذكر الوالدة لأن حقها أكثر فدعاؤها أولى بالإجابة (مرقاة المفاتيح 4/1535)

[2] سنن الترمذي، الرقم: 3598، وقال: هذا حديث حسن

[3] سنن أبي داود، الرقم: 1535، سنن الترمذي، الرقم: 1980، وقال: هذا حديث غريب لا نعرفه إلا من هذا الوجه والأفريقي يضعف في الحديث

[4] سنن ابن ماجه، الرقم: 2893، وإسناده حسن كما في مصباح الزجاجة فى زوائد ابن ماجة 3/183

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …