Uadilifu Wa Ali (radhiya allaahu ‘anhu)

Ali bin Rabi’ah anasimulia kwamba wakati mmoja, Ja’dah bin Hubairah (radhiya allaahu ‘anhu) alikuja kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) na akasema, “Ewe Ameer-ul-Mu’mineen! Tunakuta watu wawili wanakujia (na ugomvi wao). Moja kati ya hao wawili wewe ni kipenzi zaidi kwake kuliko hata familia yake na mali yake, alafu yule mwingine kama angeweza kukuchinja basi angefanya hivyo (kwa uadui wake kwako). Lakini, licha ya hayo, unatoa hukumu kumpendelea yule anayekuchukia na sio yule anayekupenda!”

Aliposikia hivyo, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alipiga kidogo kifua cha Ja’dah (radhiya allaahu ‘anhu) na mkono wake (kutokana na mapenzi na ili kuvuta mazingatio yake kwa yale aliyokuwa akitaka kumwambia) kisha akasema, “Lau hukumu ingekuwa kupitia uhusiano nilionao na watu, basi mimi ningeweza kuamua kwa niaba ya yule ninayemtaka. Lakini, hukumu inatokana na amri ya Allah Ta‘ala (na katika kumpendelea yule aliye juu ya haq. Kwa kuwa mtu anayenichukia yupo kwenye haq, itabidi nitoe hukumu upande wake).” (Al-Bidaayah Wan-Nihaayah 11/108)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …