Mapenzi Ya Dhati Ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu)

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) anaripoti:

Kuna wakati moja, nilikuwa mgonjwa. Nikiwa mgonjwa, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuja kunitembelea. Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipoingia nyumbani kwangu, nilikuwa nimejilaza. Aliponiona niko katika hali hio, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alinikaribia na kuvua kitamba aliyokuwa ameivaa kisha akanifunika nacho. Baada ya hapo, alipoona udhaifu wangu, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisimama na akaenda msikitini kuswali nafl. Baada ya kuswali, alimuomba Allah Ta’ala anibariki na shifaa.

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akanijia na kuchukuwa kitamba chake na akaniambia: “Simama ewe mtoto wa Abu Taalib, kwa sababu umeponywa!” Nilisimama na kujikuta nimepona kabisa. Nilijikuta katika hali ambayo hakuna dalili ya ugonjwa au udhaifu uliobaki katika mwili wangu.

Kisha Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akasema: “Kila nilipomuomba Allah Ta’ala, alikubali dua yangu na akanipa nilichokuwa nimekiomba. (Katika kipindi hiki) chochote nilichojiulizia mwenyewe, pia nilikuombea wewe, (pamoja na shifaa yako).” (Fadhaa’il-ul-Khulafaa li-Abi Nu’aim #78)

Kutokana na tukio hili, tunaona mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu). Vile vile tunafahamu kuwa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) ametufundisha kupitia kitendo chake cha baraka kwamba tunapoumwa basi tumuelekee Allah Ta’ala kwenye dua tukimuomba shifaa kwa sababu kila kitu kimo ndani ya uwezo wa Allah Ta’ala.

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …