Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) na Maswali Matatu ya Mfalme wa Kirumi

Mfalme wa Warumi aliwahi kutuma kiasi kikubwa cha mali kwa Khalifa wa Waislamu. Kabla ya kuumpa Mwakilishi wake mali, Mfalme alimuamuru kuuliza maswali matatu kwa Maulamaa wa Waislamu.

Mwakilishi wa Kirumi, kama alivyoagizwa, aliuliza yale maswali matatu kwa Maulamaa lakini hawakuweza kumpa majibu ya kuridhisha.

Wakati huo, Imaam Abu Hanifa (rahimahullah) alikuwa bado mvulana mdogo na alitokea kuwepo na baba yake.

Alipoona kwamba Maulamaa hawakuweza kujibu vya kutosha yale maswali matatu, alimwendea Khalifah na kumwomba ruhusa ya kujibu maswali ya Warumi.

Khalifah alimpa ruhusa na akamgeukia Mwakilishi wa Kirumi ambaye alikuwa amekaa kwenye mimbari na aliuliza, “Je, utauliza maswali?”

Mwakilishi alipojibu kwa uthibitisho, Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akasema, “Kama ni hivyo, unatakiwa kushuka chini ili nipate kukaa kwenye mimbari.

Mwakilishi huyo alikubali na kushuka chini, akimruhusu kijana Imam Abu Hanifah (rahimahullah) kupanda.

Mwakilishi wa Kirumi kisha akauliza swali lake la kwanza, “Ni kitu gani kilikuwepo kabla ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)?”

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) alijibu kwa kuuliza swali. “Je, Unajua hesabu?” Mwakilishi akajibu, “Ndiyo.”

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akaendelea, “Ni nini kinachotangulia kabla ya namba ‘moja’?” Mwakilishi akajibu, “Moja ndio namba ya kwanza; hakuna kitu kabla yake.”

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akamalizia jibu lake akieleza: “Ikiwa hakuna kitu kabla ya namba ya kwanza ya mithali, inawezaje kuwa kuna chochote kabla ya Aliye Halisi (Mwenyezi Mungu subhaanahu wata’aala)?”

Mwakilishi kisha akauliza swali la pili. Aliuliza, “Mwenyezi Mungu anaelekea upande gani?”

Kwa mara nyingine tena, Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akajibu kwa kuuliza swali lake mwenyewe, “Unapowasha taa, nuru huangaza upande gani?” Mwakilishi akajibu, “Nuru inang’aa kwa usawa katika pande zote nne.”

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akaeleza, “Ikiwa nuru inayoweza kuwashwa na kuzimwa haijazuiliwa na kuwekewa mipaka na mwelekeo, vipi nuru ya Muumba wa mbingu na ardhi, ambayo ni ya milele na yenye nguvu, itazuiliwa na kuwekewa mipaka na mwelekeo.?”

Kisha mwakilishi huyo akauliza swali lake la tatu na la mwisho, “Allah anafanya nini?”

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akajibu: “Amemteremsha kafiri kama wewe kutoka kwenye mimbar na akamuinua Muumini kama mimi kutoka chini.”

Imam Abu Hanifah (rahimahullah) alijibu kwa usahihi na kwa ufasaha maswali yote matatu na mwakilishi wa Kirumi alikiri kushindwa na akaondoka.

Majadiliano Baina Ya Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) Na Kundi La Watu Ambao Hawamuamini Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)

Kuna wakati fulani kundi la makafiri lilimwendea Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) kwa nia mbaya ya kumuua.

Pindi alikutana nao, Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) aliamua kujihusisha katika mazungumzo na kuwauliza:

“Ikiwa mtu kadai kwamba aliona meli ambayo haikuwa na kapteni wala mabaharia wa kuiongoza na kuielekeza, meli ikipita kati ya mawimbi ya bahari katika mstari ulionyooka kabisa, ikijipakia bidhaa kutoka pwani moja hadi sehemu nyingine, na kufanya haya yote peke yake bila mtu wa kuisimamia na kuidhibiti, ungesemaje?”

Hapo hapo kundi hicho lilisema kwa mshangao, “Jambo kama hilo halina mantiki kiasi kwamba hakuna mtu mwenye akili ambaye atakubali jambo hilo kuwezekana!”

Imaam Abu Hanifah (rahimahullah) akajibu akisema, “basi akili zenu zimepatwa na nini? Unapokubali kwamba meli moja haiwezi kusafiri na kufanya kazi bila mabaharia ndani, basi unakubali vipi kwamba ulimwengu wote unaweza kufanya kazi bila ya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) kuudhibiti?”

Kundi nzima lilishangazwa na hoja hii na mara moja wakatubu na kuukubali Uislamu mikononi mwa Imaam Abu Hanifah (rahimahullah).

About admin

Check Also

Rizki Ipo Mikononi Wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Peke Yake

Kila kiumbe anahitaji rizki kwa ajili ya kuendelea kwake na kuishi kwake, na rizki iko …