Ushujaa Wa Ali (radhiyallahu ‘anhu) Katika Vita Vya Khaibar

Katika tukio la Khaibar, baada ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kukabidhi bendera ya Uislamu kwa Ali (radhiya allaahu anhu), Ali (radhiyallahu anhu) aliliongoza jeshi la Maswahaabah (radhiyallahu anhu) hadi kwenye ngome ya Qamoos.

Walipokaribia ngome, shujaa mmoja wa kiyahudi, jina lake Marhab, alitoka ili kuwapinga (waislamu). Marhab alikuwa shujaa maarufu ambaye alijisifika kwa nguvu zake nyingi na ushujaa. Hivyo basi, pale Marhab alipokabiliana na ‘Ali (radhiya allaahu anhu) na Waislamu, alianza kujifakharisha juu ya ushujaa wake mkubwa katika vita kwa kusema mashairi yafuatayo:

قَدْ عَلِمَتْ خَيْبَرُ أَنِّيْ مَرْحَبُ

Watu wa Khaibar wote wanajua vizuri kwamba mimi ni Marhab

شَاكِيْ السِّلَاحِ بَطَلٌ مُجَرَّبُ

Mimi ni shujaa ambaye nina silaha za kutosha na uzoefu wa vita

إِذَا الْحُرُوْبُ أَقْبَلَتْ تَلَهَّبُ

(Ninaonyesha nguvu na ushujaa wangu wa kweli) wakati ambapo mapigano yanaanza na vita kuzidi.

Kwa kusema maneno haya, alitoa changamoto kwa Waislamu kujitokeza na kupigana naye. Kwa kujibu changamoto lake, ‘Aamir bin Akwa’ (radhiya allaahu anhu) akatoka. ‘Aamir (radhiya allaahu ‘anhu) alikutana na Marhab na akasema mashairi yafuatayo:

قَدْ عَلِمَتْ خَيْبَرُ أَنِّيْ عَامِرُ

Watu wa Khaibar wote wanajua vizuri kwamba mimi ni Aamir

شَاكِيْ السِّلَاحِ بَطَلٌ مُغَامِرُ

Mimi ni shujaa ambaye nina silaha kamili na niko tayari kutumbukia katika vita yoyote ile

Mapambano yalianza na Marhab alipiga kwanza. Aliupeleka upanga wake kumuelekea ‘Aamir (radhiya allaahu anhu), ambaye alizuia kipigo hicho na ngao yake. Pigo la upanga wa Marhabu lilikuwa na nguvu sana kiasi kwamba lilipoipiga ile ngao, likaingia ndani yake. ‘Aamir (radhiya allaahu anhu) alichukua fursa hii kumpiga Marhab kutoka chini ya ngao yake. Hata hivyo, alimkosa Marhab na upanga wake ukamrudia, ukampiga na kumsababishia jeraha mbaya.

Baada ya hapo, ‘Ali (radhiya allaahu anhu) akatoka kwenda kupambana na Marhab. Marhab tena akasoma mashairi zile zile, ambazo ‘Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alijibu kwa kusema yafuatayo:

أَنَا الَّذِيْ سَمَّتْنِيْ أُمِّيْ حَيْدَرَهْ

Mimi ndiye ambaye mama yake alimwita Haydar (Simba Mkali)

كَلَيْثِ غَابَاتٍ كَرِيْهِ الْمَنْظَرَهْ

Kama simba anayeonekana mkali wa msituni

أُوْفِيْهِمْ بِالصَّاعِ كَيْلَ السَّنْدَرَهْ

Inaponibidi kubadilishana, basi natoa kipimo kamili (yaani pigo langu limekamilika na ninamuua adui haraka na mara moja)

Kuhusu Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kujiita Haydar (simba mkali), imepokewa kwamba alipozaliwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) baba yake Abu Taalib alitoka safarini. na hakuwepo Makka Mukarramah. Kwa hiyo, mama yake akamwita Haydar (maana yake simba). Aliimpa jina la Haydar baada ya baba yake, ambaye jina lake lilikuwa Asad (maana yake pia simba). Abu Taalib aliporudi Makka Mukarramah kutoka safarini na mkewe akamjulisha kwamba amempa mtoto jina la haydar, alibadilisha jina na kumwita mwanawe kwa jina la ‘Ali. Baada ya hapo, ‘Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alijulikana sana na jina alilopewa na baba yake. lakini, katika tukio hili, alijitaja mwenyewe kwa kutumia jina alilopewa na mama yake.

Katika riwaaya moja, Marhab aliota ndoto usiku uliotangulia ambapo aliona kwamba alikuwa ameraruliwa na simba. ‘Allaamah Zurqaani (rahimahullah) ametaja kwamba ‘Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alibarikiwa na elimu hii kupitia kashf (kuonyeshwa, ima kwa ndoto au kwa njia nyingine). Ni kwa sababu hii alijitaja mwenyewe kwa kutumia jina la Haydar, ambalo lilimaanisha simba mkali, katika shairi lake. Kujitambulisha mwenyewe kama simba mkali, Marhab alitambua kwamba ndoto yake iliashiria juu yake kukutana na mwisho wake kupitia upanga wa ‘Ali (radhiya allaahu ‘anhu). Hii ilimfanya aingiwe na hofu na kupoteza ujasiri.

Kisha wakaanza kupigana, na kwa kipigo kimoja tuu, ‘Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alipasua fuvu la kichwa la Marhab, bingwa ‘maarufu’ wa Khaibar, na akakatisha maisha yake. Kisha Allah Ta’ala akambariki ‘Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kwa kuiteka ngome hii. (Sahih Bukhaari #4210, Sahih Muslim #1807, Majma’uz Zawaa’id #10206, Fat-hul Baari 7/535-549, Sharhun Nawawi juzuu ya 12 safha ya 185 na Sharhuz Zurqaani 3/244-258)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …