Hofu Ya Ali (radhiya allaahu ‘anhu) Na Akhera

Kumail ibn Ziyad (rahimahullah) anaripoti yafuatayo:

Wakati mmoja, nilifuatana na Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alipokuwa akitoka katika mji wa Kufah na kuelekea Jabbaan (kijiji nje ya Kufah). Alipofika Jabbaan, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) aligeuka kuelekea makaburini na akaita, “Enyi wakazi wa makaburini! Enyi watu ambao miili yenu imeoza! Enyi watu wa upweke! Je, hali yenu ikoje? Hali yetu (hapa duniani) ni kwamba mali za marehemu zimekatwa na kugawanywa, watoto wa marehemu wamekuwa yatima na wanandoa wa marehemu sasa wameolewa tena! Hii ndiyo hali yetu, basi tujulishe hali yenu (makaburini)?”

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akanigeukia na kusema, “Ewe Kumail! Lau wenyeji wa makaburi haya wangeruhusiwa na Allah Ta’ala kuitikia wito wetu, wangesema: “Riziki bora (ya Akhera) ni taqwa.”

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kisha akaanza kulia na kusema, “Ewe Kumail! Kaburi, kwa kweli, ni sanduku ambalo lina vitendo vya mtu. Ni wakati wa kufa tu ndipo mtu atagundua ni matendo gani amepeleka mbele na yakimngojea kaburini mwake (yaani. hali ya mtu katika kaburi lake – ima adhabu au faraja – itaamuliwa na matendo atakazokwenda nazo pamoja naye kwenye ulimwengu ujao).(Taareekh Dimashq 50/251)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …