Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) Amemchagua Ali (radhiya allaahu ‘anhu) Kuisimamia Madinah Munawwarah

Katika tukio la Vita vya Tabook, wakati Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alipokuwa anaondoka kutoka Madinah Munawwarah, alimchagua Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kusimamia mambo ya Madinah Munawwarah akiwa hayupo.

Kwa hiyo, kwa maelekezo ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), Ali (radhiya allaahu ‘anhu) hakutoka na jeshi, bali alibakia Madinah Munawwarah.

Baada ya hapo, baadhi ya watu walianza kueneza uzushi kwamba sababu ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kumwambia Ali (radhiya allaahu ‘anhu) abaki nyuma ni kwamba amechukizwa naye. Aliposikia hivyo, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) mara moja akaja kwa Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) na akamtajia yale watu walikuwa wakiyasema.

Kwa mujibu wa riwaya moja, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alimwambia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Sitaki Waarabu waseme kuhusu mimi, ‘Amemwacha binamu yake (Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) na akabaki nyuma.”

Zaidi ya hayo, ilikuwa ni hamu kubwa ya Ali (radhiya allaahu ‘anhu) kujiunga na jeshi ili aweze kutekeleza amali ya Jihadi katika njia ya Allah Ta’ala. Kwa mujibu wa riwaya nyingine, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) alimwambia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam), “Ewe Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Je, unaniacha nyuma na wanawake na watoto?”

Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akamtuliza na kumwambia, “Je, hufurahi kwamba nafasi yako pamoja nami utakuwa kama msimamo wa Harun kwa Musa (alaihimas salaam) isipokuwa kwamba hakutakuwa na Nabii atakayekuja baada yangu? ”

Kwa maneno mengine, wakati Nabii Musa (‘alayhis salaam) alipokwenda Mlima wa Toor, alimwacha kaka yake, Nabii Haroon (‘alaihis salaam), katika kuwasimamia watu. Hii iliashiria cheo cha juu cha Nabii Haroon (‘alayhis salaam) na imani ambayo Nabii Musa (‘alayhis salaam) alikuwa nayo kwake.

Vile vile Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alimfahamisha Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba kumchagua yeye kusimamia mambo ya Madinah Munawwarah akiwa hayupo ni dalili kwamba Rasulullah (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ana imani naye.

Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliposikia hayo, mara moja alisema: “Nimefurahi, nimefurahi (kwa maamuzi wa Allah Taala na Mtume Wake (Sallallahu ‘alaihi wasallam)).

About admin

Check Also

Nafasi Ya Juu Ya Abu Ubaidah (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mbele Ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)

Baada ya kufariki kwa Mtume (Sallallahu alaihi wasallam), Ma answaar walikuwa wamekusanyika huko Thaqifah Bani …