Fadhila za Dua

Malaika Akimuombea Dua Anayemuombea Ndugu Yake Dua

Abud Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa akisema: “Dua anayoifanya Muislamu kwa ajili ya ndugu yake wakati hayupo inakubaliwa. Kila anapoomba dua kwa ajili ya wema ya ndugu yake, kuna Malaika ambaye amechaguliwa kusimama kichwani kwake. Malaika huyo husema Aamin kwa dua yake na Malaika akimuombea dua kwa kusema: “Allah Ta’ala akujalie mfano wa ulichomwombea ndugu yako.”[1]

Fadhila Ya Kuwaombea Waumini Dua

Imepokewa kutoka kwa Abud Dardaa (radhiyallahu ‘anhu) kwamba alimsikia Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) akisema: “Mwenye kuwaombea waumini wanaume na wanawake msamaha kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) mara ishirini na tano au mara ishirini na saba kila siku, atakuwa katika wale ambao ni mustajaabud da’waat (yaani wale ambao dua zao zimekubaliwa na Mwenyezi Mungu) na atakuwa miongoni mwa waja hao wema ambao kwa sababu ya matendo yao mema Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) anateremshia ulimwengu rizki.”[2]


[1] صحيح مسلم، الرقم: 2733

[2] رواه الطبراني وفيه عثمان بن أبي العاتكة وقال فيه: حدثت عن أم الدرداء وعثمان هذا وثقه غير واحد وضعفه الجمهور وبقية رجاله المسمين ثقات كذا في مجمع الزوائد، الرقم: 17600

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …