Fadhila za Dua

Anayefanya Dua Siku zote Anafaidi

Abu Sa’eed Khudri (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Muislamu yoyote akimuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) na kumnyenyekea, na dua yake haina dhambi yoyote (yaani kuomba jambo lolote lisiloruhusiwa) au kukata mahusiano ya kifamilia, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) atamjaalia moja katika mambo matatu. Ama Atampa aliyoyaomba (katika dunia hii), au Amhifadhie malipo ya dua yake katika aakhirah, au amwondoshee balaa.” Maswahaabah (radhiyallahu ‘anhum) wakasema, “Katika hali hiyo, tutashiriki katika dua kwa wingi.” Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akajibu, “Allah Ta’ala ni zaidi kwa kila kitu (yaani Nguvu zake na hazina yake ni zaidi kwa kile unachokiomba).[1]

Njia Ya Baraka Katika Rizki Na Kulindwa Na Maadui

Jaabir bin Abdillah radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliwaambia Maswahabah (radhiyallahu ‘anhum): “Je, nisiwaonyeshe njia ambayo mtaokolewa kutoka kwa maadui zenu na mtapata rizki kwa wingi? Rejea kwa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) katika dua usiku na mchana, kwani dua ni silaha ya Muumini.”[2]


[1] مسند أحمد، الرقم: 11133، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17210: رواه أحمد وأبو يعلى بنحوه والبزار والطبراني في الأوسط ورجال أحمد وأبي يعلى وأحد إسنادي البزار رجاله رجال الصحيح غير علي بن علي الرفاعي وهو ثقة

[2] مسند أبي يعلى الموصلي، الرقم: 1812، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17199: رواه أبو يعلى وفيه محمد بن أبي حميد وهو ضعيف

About admin

Check Also

Dua Baada Ya Kula 1

Dua ya kwanza: Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alitupa chakula na vinywaji na kutufanya Waislamu.

Dua ya pili Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alinipa chakula hiki kula, na alinipa bila juhudi yoyote au jitihada kutoka upande wangu.

Maelezo: Mu'aadh bin Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, "Yoyote anayekula chakula chochote na baada ya hapo anasoma Dua iliyotajwa hapo juu, dhambi zake zilizopita na za baadaye (ndogo) zitasamehewa. "