binary comment

Fadhila za Dua

Silaha Ya Muumini

Ali (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema, “Dua ni silaha ya Muumini, nguzo ya Dini, na nuru ya mbingu na ardhi.”[1]

Dua Ni Asili ya Ibaadah

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Dua ndio asili ya ibaadah.”[2]

Allah Ta’ala Hufurahishwa na Mja Anapo omba Dua

Aaishah (radhiyallahu ‘anha) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Hakika Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Anawapenda wale wanaomuomba Yeye daima.”[3]

Katika riwaya ya Tirmidhi iliyopokelewa na Abu Hurairah (radhiyallahu ‘anhu), Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) ametaja: “Mtu asiyemuomba Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), basi Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) humkasirikia.”[4]

Dua Humnufaisha Mtu Kwa Sasa na pia Wakati Ujao

Ibnu Umar (radhiyallahu ‘anhuma) anaripoti kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “Dua ina manufaa kwa sasa na kwa siku zijao. Kwa hivyo, enyi waja wa Allah Ta’ala, dumuni katika kufanya dua.”[5]


[1] المستدرك للحاكم، الرقم: 1812، وقال الحافظ في إتحاف المهرة (الرقم: 14167):كم في الدعاء: … وقال: صحيح فإن محمد بن الحسن هو ابن التل وهو صدوق

[2] سنن الترمذي، الرقم: 3371، وقال: هذا حديث غريب من هذا الوجه لا نعرفه إلا من حديث ابن لهيعة

[3] أخرجه الطبراني في الدعاء بسند رجاله ثقات إلا أن فيه عنعنة بقية عن عائشة مرفوعا إن الله يحب الملحين في الدعاء كذا في فتح الباري 11/95

[4] سنن الترمذي، الرقم: 3373، وحديثه رفعه من لم يسأل الله يغضب عليه أخرجه أحمد والبخاري في الأدب المفرد والترمذي وابن ماجه والبزار والحاكم كلهم من رواية أبي صالح الخوزي بضم الخاء المعجمة وسكون الواو ثم زاي عنه وهذا الخوزي مختلف فيه ضعفه بن معين وقواه أبو زرعة (فتح البارى 11/95)

[5] سنن الترمذي، الرقم: 3548، وقال: هذا حديث غريب لا نعرفه إلا من حديث عبد الرحمن بن أبي بكر القرشي وهو المكي المليكي وهو ضعيف في الحديث قد تكلم فيه بعض أهل الحديث من قبل حفظه

About admin

Check Also

Dua Baada Ya Kula 1

Dua ya kwanza: Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alitupa chakula na vinywaji na kutufanya Waislamu.

Dua ya pili Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata'ala) ambaye alinipa chakula hiki kula, na alinipa bila juhudi yoyote au jitihada kutoka upande wangu.

Maelezo: Mu'aadh bin Anas (Radhiyallahu anhu) anaripoti kwamba Rasulullah (Sallallahu alaihi wasallam) alisema, "Yoyote anayekula chakula chochote na baada ya hapo anasoma Dua iliyotajwa hapo juu, dhambi zake zilizopita na za baadaye (ndogo) zitasamehewa. "