Dua ya Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) kwa Ali (radhiya allaahu ‘anhu) wakati wa Kumtuma kwenda Yemen

Ali (radhiya allaahu ‘anhu) anaripoti:

Rasulullah (sallallahu ‘alahi wasallam) alinituma kama waziri wake kwenda Yemen. Kabla ya kuondoka, nilimwambia, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (sallallahu ‘alaihi wasallam)! Unanipeleka kwa watu ambao ni wakubwa kuliko mimi. Zaidi ya hayo, mimi ni kijana na sina ufahamu wowote katika uwanja wa Qadhaa (mambo ya mahakama na kuhukumu).”

Aliposikia wasiwasi wangu, Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) aliweka mkono wake uliobarikiwa juu ya kifua changu na akaomba dua kwa maneno yafuatayo:

اللهم ثبت لسانه واهد قلبه

Ewe Mwenyezi Mungu! Uthibitishe ulimi wake (katika kusema kweli) na uongoze moyo wake (kwenye haqq)!

Baada ya hapo, Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) akampa nasaha na kusema: “Ewe Ali! Kama watu wawili wanaogombana wamekaa mbele yako, basi hakikisha kwamba hutoi hukumu yoyote baina yao mpaka uisikilize kesi ya upande wa pili kama jinsi ulivyosikiliza kesi ya upande wa kwanza. Ukishikilia ushauri wangu huu, utaelewa hali ipasavyo, na utajua jinsi ya kuamua na kutoa hukumu kati yao.”

Imepokewa kwamba kwa ajili ya Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) kumuombea Ali (radhiya allaahu ‘anhu) dua hii na kumpa nasaha hizi, Ali (radhiya allaahu ‘anhu) hakuwahi kukumbana na ugumu wowote wakati wa kutoa hukumu baina ya watu.” (Musnad Ahmed #882)

About admin

Check Also

Mshale Wa Kwanza Kurushwa kwa Ajili Ya Uislamu

Sa’d (radhiya allaahu ‘anhu) alikuwa miongoni la kundi la Maswahabah ambao Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) …