Dua

Dua ni njia ambayo mja huchota kutoka katika hazina zisizo na mipaka za Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala). Kuna fadhila nyingi zilizoripotiwa ndani ya Hadith kwa wale wanao omba dua. Mtume (sallallahu ‘alaihi wasallam) amesema kwamba dua ni asili ya ibaadah zote.[1] 

Katika Hadith nyingine, Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) ametaja kuwa Allah Ta’ala humridhia mja anayeomba dua na kumuomba kwa haja zake,[2]  na Allah Ta’ala humkasirikia mja asiyerejea Kwake katika dua, kumuomba mahitaji yake.

Kwa ujumla, katika ulimwengu, watu wamkasiria na kupoteza heshima kwa mtu anayeendelea kuomba msaada kwao. Lakini Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), Muumba wa ulimwengu, mapenzi yake kwa waja wake hayana mipaka. Hivyo basi, Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) anawaamrisha waja Wake kuendelea kurejea kwake katika dua na huwa radhi nao wanapomuomba.[3] 

Kwa hivyo, ni muhimu sana kwa muumini kufanya dua kuwa miongoni ya ratiba yake kila siku, ili kutafuta neema za Allah Ta’ala katika mambo yake yote na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yake yote.


[1] سنن الترمذي، الرقم: 3371، وقال: هذا حديث غريب من هذا الوجه لا نعرفه إلا من حديث ابن لهيعة

[2] أخرجه الطبراني في الدعاء بسند رجاله ثقات إلا أن فيه عنعنة بقية عن عائشة مرفوعا إن الله يحب الملحين في الدعاء كذا في فتح الباري 11/95

[3] سنن الترمذي، الرقم: 3373، وحديثه رفعه من لم يسأل الله يغضب عليه أخرجه أحمد والبخاري في الأدب المفرد والترمذي وابن ماجه والبزار والحاكم كلهم من رواية أبي صالح الخوزي بضم الخاء المعجمة وسكون الواو ثم زاي عنه وهذا الخوزي مختلف فيه ضعفه بن معين وقواه أبو زرعة (فتح البارى 11/95)

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …