Kumtambua Allah Ta’ala

Allah Ta’al Ndiye Muumba na Mlinzi wa kila kiumbe katika ulimwengu. Kila kitu katika ulimwengu, iwe ni galaksi, mfumo wa jua, nyota, sayari, au ardhi na kila kilichomo ndani yake, ni viumbe vya Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala).

Yule anayetafakari juu ya ukubwa na uzuri wa viumbe hawa wote basi afikirie ukubwa na uzuri wa aliyeviumba utakuwaje!

Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Anatualika, katika Quraan Takatifu, kutafakari juu ya viumbe vyake na kwa hivyo kutambua ukubwa na uwezo Wake. Allah Ta’ala Anasema:

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ‎﴿١٩٠﴾‏ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ‎﴿١٩١﴾

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) wakiwa wamesimama au wamekaa au wamelala ubavuni, na wakatafakari kuumbwa kwa mbingu na ardhi, (wakisema) Mola wetu! Hukuumba hivi bila ya lengo; Umetakasika (kutokana na kuumba vitu bila ya makusudio), basi tulinde na adhabu ya Moto!

Imam Shafi’ee (rahimahullah) Akithibitisha Uwepo Wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)

Imepokewa kwamba mtu mmoja asiyeamuamini Allah Ta’ala aliwahi kukutana na Imaam Shaafi’ee (rahimahullah) na akamuomba uthibitisho kuhusu uwepo wa muumba, Allah Ta’ala.

Imam Shafi‘ee (rahimahullah) akamjibu hapo hapo, “Angalia majani ya mulberry. Rangi, ladha, harufu, muundo na sifa za kila jani ni sawa.

“Licha ya kuwa sawa kabisa, ikiliwa na mdudu hariri, hariri Inatoka. Nyuki na yeye anapokula yale majani, asali hutolewa. Inapoliwa na mbuzi, kinyesi hutolewa na wakati inapoliwa na kulungu, miski hutolewa.

“Ni kazi pekee ya muumba ambaye ni wa milele na mwenye uwezo wote unaweza kusababisha vitu vingi tofauti-tofauti kutengenezwa kutoka kitu kimoja. La sivyo, mantiki na ufahamu ungedai kwamba mwisho wa vitu vyote viwe sawa sawa kwa sababu viliyoingia vyote vilikuwa sawa sawa.”

Imam Malik (rahimahullah) Akithibitisha Uwepo Wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala)

Mtu mmoja alikuja kwa Imam Malik (rahimahullah) na kumuuliza atoe uthibitisho wa uwepo wa muumba.

Imam Malik (rahimahullah) akajibu, “Angalia uso wa mtu. Ingawa inaweza kuwa ndogo, lakini uso wa kila mtu una macho, pua, masikio, ulimi, mashavu, fizi n.k.

“Licha ya kila uso kuwa na viungo sawa, hakuna uso mbili zinazofanana kabisa kwa sura na umbo. Sauti ni tofauti na viungo pia ni tofauti.”

“Ukamilifu huu ambao kila mtu amebarikiwa nao unaweza tu kuwa matokeo ya kazi ya muumba.”

Ishara Zinazoonyesha Kuna Muumba

Bedui mmoja aliwahi kusema shairi ifuatao:

البعرة تدل على البعير     وآثار الأقدام على المسير

فسماء ذات أبراج وأرض ذات فجاج     كيف لا تدل على اللطيف الخبير

Kinyesi na choo linaonyesha kuwa ngamia ilipita na nyayo zinaonyesha kuwa mtu amepita,

basi itakuwaje mbingu iliyojaa na nyota na ardhi iliyopitiwa na njia isionyeshe uwepo wa Muumba ambaye ni Mwingi wa Rehma na mwenye kufahamu yote?

Hivyo basi, baada ya kutambua uwezo na ukuu wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala), mtu anapaswa kutafakari juu ya mapenzi yake ya kina kwa Muumba wake. Licha ya kum’aasi na kutostahili kwetu, bado anaendelea kutubariki kwa fadhila na neema zisizohesabika, usiku na mchana.

Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Atujaalie tuwe na uwezo wa kurejea Kwake na kuendelea kuwa watiifu kwake kila wakati.

About admin

Check Also

Rizki Ipo Mikononi Wa Mwenyezi Mungu (subhaanahu wata’aala) Peke Yake

Kila kiumbe anahitaji rizki kwa ajili ya kuendelea kwake na kuishi kwake, na rizki iko …