Sura Maalum Kwenye Nyakati na Matukio Mbalimbali 5

10. Soma Sura Fatiha na Sura Ikhlaas kabla ya kulala.

Anas (radhiyallahu ‘anhu) anasema kwamba Mtume (Sallallahu ‘alaihi wasallam) alisema, “(Wakati wa kulala,) unapoweka ubavu wako juu ya kitanda, na ukasoma Sura Faatihah na Sura Ikhlaas, basi utasalimika na kila kitu isipokuwa kifo.”[1]

11. Soma Surah Zumar na Surah Bani Israaeel kabla ya kulala.

Abu Lubaabah (radhiyallahu ‘anhu) anaripoti kwamba Aaishah (radhiyallahu ‘anha) alisema, “Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa halali mpaka asome Sura ya Zumar na Surah Bani Israaeel.[2]

12. Soma Musabbihaat (yaani hizo surah zinazoanza na maneno ya tasbeeh) kabla ya kulala. Sura hizi ni Surah Bani Israaeel, Surah Hadeed, Surah Hashr, Surah Saff, Surah Jumu’ah, Surah Taghaabun na Surah A’laa.

Irbaadh bin Saariyah (radhiyallahu ‘anhu) anasimulia kwamba Rasulullah (sallallahu ‘alaihi wasallam) alikuwa hawezi kulala mpaka asome Musabbihaat, na angesema: “Katika Sura hizi, kuna Aya kubwa zaidi kuliko Aya elfu moja.[3]


[1] مسند البزار، الرقم: 7393، وقال العلامة الهيثمي رحمه الله في مجمع الزوائد، الرقم: 17030: رواه البزار وفيه غسان بن عبيد وهو ضعيف ووثقه ابن حبان وبقية رجاله رجال الصحيح

[2] سنن الترمذي، الرقم: 3405، 2920، وقال: هذا حديث حسن غريب

[3] سنن الترمذي، الرقم: 3406، وقال: هذا حديث حسن غريب

About admin

Check Also

Sunna Na Adabu Za Dua 8

19. Jiepushe na ulaji wa haramu au chakula chenye mashaka na kujihusisha na madhambi. Mtu …